Kocha wa Chelsea Jose Mourinho |
Jose Mourinho amesisitiza kuwa Mabingwa Watetezi Manchester United hawapo nje ya mbio za Ubingwa na bado ni Timu hatari.
Jumapili, Uwanjani Stamford Bridge, Chelsea inaikaribisha Man United kwenye Mechi ya Ligi Kuu England huku Man United wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Arsenal na Pointi 9 nyuma ya Chelsea ambao wako Nafasi ya 3.
Lakini Mourinho anaamini bado wana nafasi ya kutetea Ubingwa wao na amesema: “Arsenal na Manchester City ndio Timu za juu. City wana silaha na Liverpool wana nafasi murua kwa sababu hawachezi Ulaya. Man United ni Man United. Pointi 11 ni pengo kubwa lakini naamini watapigana hadi mwisho. Tunacheza dhidi ya Mabingwa. Tunacheza na Manchester United, sio Timu iliyo Pointi 11 nyuma ya Vinara!”
Aliongeza: “Nimecheza Mechi nyingi kubwa na unazoefu wangu unaniambia hivyo. Timu ambayo inaonekana ipo kwenye matatizo ndio Timu hatari.”
++++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU:
-Chini ya Jose Mourinho, katika himaya zake mbili kama Meneja, Chelsea haijafungwa hata Mechi moja ya Ligi Uwanjani Stamford Bridge!
++++++++++++++++++++++++++
Vile vile Mourinho amekataa kumwonea imani David Moye, Meneja wa Man United, na kudai yupo salama na kwenye Klabu ambayo haiyumbi.
Amesema: “Klabu imempa imani kubwa. Ni Klabu yenye utamaduni mzuri inayoamini Mameneja wake. Atapata muda wa kujenga Timu yake.”
Kuhusu Timu yake, Mourinho amesema yeye hana mchecheto na kutwaa Ubingwa bali kazi yake kubwa ni kuijenga Chelsea ya baadae.
Pia Mourinho alidokeza kuwa Mchezaji wao mpya, Nemanja Matic, hataanza Mechi ya Jumapili lakini Frank Lampard huenda akacheza baada kutocheza tangu Siku ya Mwaka mpya.
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
P |
GD |
PTS |
1 |
Arsenal |
21 |
22 |
48 |
2 |
Man
City |
21 |
36 |
47 |
3 |
Chelsea |
21 |
21 |
46 |
4 |
Liverpool |
21 |
25 |
42 |
5 |
Everton |
21 |
15 |
41 |
6 |
Tottenham |
21 |
1 |
40 |
7 |
Man
United |
21 |
11 |
37 |
8 |
Newcastle |
21 |
2 |
33 |
9 |
Southampton |
21 |
4 |
30 |
10 |
Hull |
21 |
-5 |
23 |
11 |
Aston
Villa |
21 |
-7 |
23 |
12 |
Stoke |
21 |
-13 |
22 |
13 |
Swansea |
21 |
-4 |
21 |
14 |
West
Brom |
21 |
-5 |
21 |
15 |
Norwich |
21 |
-18 |
20 |
16 |
Fulham |
21 |
-24 |
19 |
17 |
West
Ham |
21 |
-10 |
18 |
18 |
Cardiff |
21 |
-18 |
18 |
19 |
Sunderland |
21 |
-15 |
17 |
20 |
Crystal
Palace |
21 |
-18 |
17 |
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Januari 18
1545 Sunderland v Southampton
1800 Arsenal v Fulham
1800 Crystal Palace v Stoke
1800 Man City v Cardiff
1800 Norwich v Hull
1800 West Ham v Newcastle
2030 Liverpool v Aston Villa
Jumapili Januari 19
1630 Swansea v Tottenham
1900 Chelsea v Man United
Jumatatu Januari 20
2300 West Brom v Everton
Jumanne Januari 28
2245 Man Utd v Cardiff
No comments:
Post a Comment