![]() |
| IGP Ernest Mangu |
![]() |
| Naibu IGPAbdulrahman Kaniki |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete leo (jana), Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna
wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.
Taarifa iliyotolewa usiku wa leo(jana) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.
Taarifa iliyotolewa usiku wa leo(jana) na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini anayestaafu, Saidi Mwema.
Kabla ya uteuzi wake unaoanza
keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa Mkurugenzi wa
Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence)katika Jeshi hilo la
Polisi.
Aidha, taarifa hiyo inasema kuwa Rais
Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi,
ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa wa Jeshi la Polisi.
Kabla ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki
alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner for Forensic
Investigations).
Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment