LIGI
KUU ENGLAND-TATHMINI MECHI ZA BOKSING DEI!
MAN CITY Vs LIVERPOOL
NI BOKSING DEI, lakini huko England
Timu zote 20 za Ligi Kuu England Alhamisi Desemba 26 zipo kilingeni
kucheza Mechi 10 na fungua dimba ni Mechi ya Mabingwa Watetezi Manchester
United watakaokuwa huko KC Stadium kuivaa Hull City, na baadae Jioni kufuata
Mechi 8 na Usiku ndio ule Mtanange, Bigi Mechi, huko Etihad kati ya Man City na
Vinara wa Ligi Liverpool.
PATA
DONDOO/TATHMINI/HALI ZA WACHEZAJI MECHI KWA MECHI:
++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
Alhamisi Desemba 26
[Saa za Bongo]
1545 Hull v Man United
1800 Aston Villa v Crystal Palace
1800 Cardiff v Southampton
1800 Chelsea v Swansea
1800 Everton v Sunderland
1800 Newcastle v Stoke
1800 Norwich v Fulham
1800 Tottenham v West Brom
1800 West Ham v Arsenal
2030 Man City v Liverpool
++++++++++++++++++++++++++
HULL CITY Vs MAN U
Hull City ndio Timu yenye Rekodi nzuri
ya Difensi kwa Mechi za Nyumbani Uwanjani KC kupita Timu yeyote ya Ligi Kuu
England kwani Msimu huu wamefungwa Bao 3 tu.
Lakini Hull wanakutana na Man United
ambayo imewafunga katika Mechi zote 7 walizokutana mwisho na mara ya mwisho Man
United walishinda Bao 4-0 Mwezi Januari 2010 na Bao zote kufungwa na Wayne
Rooney.
Rooney amebakisha Goli 1 tu afikishe Bao
150 za Ligi Kuu England akiwa na Man United na kuweka Rekodi ya kuwa Mchezaji
wa Pili tu kufunga Bao hizo akiwa na Klabu moja tu, mwingine akiwa Thierry
Henry aliefunga Bao 175.
Hali za Wachezaji
Meneja wa Hull Steve Bruce, ambae ni
Mchezaji wa zamani wa Man United, huenda akachezesha Kikosi kile kile kwa Mechi
ya 4 mfululizo ya Ligi.
Hull City itawakosa Robbie Brady,
aliewahi kuwa Man United zamani, Sone Aluko na Stephen Quinn ambao ni Majeruhi.
Man United itamkosa Marouane Fellaini
ambae amefanyiwa operesheni ya mkono na pia Michael Carrick na Robin van Persie
ambao ni Majeruhi ingawa wamesharudi tena Mazoezini.
Vikosi vitatokana na:
Hull City: McGregor, Harper, Davies, Chester, Faye, Figueroa, Bruce,
Rosenior, Elmohamady, Brady, Livermore, Huddlestone, Meyler, Koren, Sagbo,
McShane, Graham, Fryatt.
Man United: De Gea, Lindegaard, Johnstone, Rafael, Smalling, Ferdinand,
Evans, Evra, Vidic, Fabio, Valencia, Nani, Jones, Fletcher, Cleverley, Giggs, Anderson,
Young, Zaha, Januzaj, Rooney, Welbeck, Kagawa, Hernandez.
Hii ni Mechi inayokutanisha Timu
zinazosuasua kwenye Ligi ingawa Villa kidogo wana afueni licha ya
kutofunga Bao hata moja katika Mechi zao 4 kati ya 5 walizocheza mwishoni
kwenye Ligi Nyumbani kwao Villa Park.
Straika Mkuu wa Villa, Christian
Benteke, sasa amefikisha Masaa 11 na Dakika 59 za Mechi za Ligi bila kufunga
Bao.
Nae Straika wa Palace, Marouane
Chamakh, amejaribu Mashuti manne tu katika Dakika 1239 za Mechi za Ligi lakini
amefunga Bao 4.
Hali za Wachezaji
Gabriel Agbonlahor anarudi Kikosini kwa
Timu ya Villa baada kutumikia Kifungo cha Mechi moja lakini Christian Benteke
huenda asiwepo kwa sababu ya maumivu ya Goti.
Villa pia itamkosa Kiungo wao Ashley
Westwood ambae yupo Kifungoni Mechi 1 baada kukusanya Kadi za Njano 5 na pia
huenda Nahodha wao, Ron Vlaar, asicheze akikabiliwa na maumivu ya Mguu.
Palace watamkosa Straika wao Marouane
Chamakh ambae yupo Kifungoni.
Vikosi vitatokana na:
Aston Villa: Guzan, Steer, Baker, Clark, Lowton, Luna, Herd, Bacuna, El
Ahmadi, Albrighton, Sylla, Tonev, Delph, Gardner, Kozak, Helenius, Weimann,
Bowery, Agbonlahor.
Crystal Palace: Speroni, Mariappa, Moxey, Ward, Gabbidon, Delaney, Bolasie,
Jedinak, Jerome, Gayle, Puncheon, Parr, Campana, Bannan, Phillips, Williams,
Price.
Cardiff City wameshinda Mechi 5
zilizopita walizocheza Nyumbani na Southampton na zote kwa tofauti ya Bao 1 tu.
Hali za Wachezaji
Cardiff City, chini ya Meneja Malky
Mackay, mwenye bifu kubwa na Mmiliki wa Klabu, Vincent Tan, anaetoka Malaysia,
huenda Ikamkosa Mkongwe Craig Bellamy ambae ana tatizo la Goti.
Southampton huenda wakawachezesha
Majeruhi wao waliopona Dani Osvaldo, Luke Shaw, Nathaniel Clyne na Kelvin
Davis, ikiwa watapita uchunguzi wa Dakika za mwisho lakini itawakosa Artur
Boruc, Victor Wanyama, anaetoka Kenya, na Guly do Prado, wote wakiwa bado na
maumivu.
Vikosi vitatokana na:
Cardiff City: Marshall, Connolly, Taylor, Caulker, Hudson, Turner,
Whittingham, Medel, Cornelius, Campbell, Odemwingie, Brayford, Kim, Smith,
Noone, Gunnarsson, Mutch, Cowie, Maynard, Theophile-Catherine, Lewis, John.
Southampton: K Davis, Gazzaniga, Cropper, Chambers, Clyne, Shaw, Fox,
Fonte, Hooiveld, Lovren, Yoshida, Cork, Schneiderlin, S Davis, Ward-Prowse,
Reed, Ramirez, Rodriguez, Lallana, Gallagher, Osvaldo, Lambert.
Chelsea Vs Swansea
Katika Mechi 3 kati ya 6 walizocheza
mwisho na Swansea City, Chelsea wamekuwa wakicheza Mtu 10 baada ya
Mchezaji wao mmoja kupewa Kadi Nyekundu.
Katika Mechi 13 walizocheza mwisho,
Swansea wameshinda 2 tu, Sare 5 na Kufungwa 6.
Jose Mourinho, Meneja wa Chelsea,
ameshinda Mechi 53 na hajafungwa hata moja katika Mechi zake 68 za Ligi
alizoisimamia Chelsea Uwanjani Stamford Bridge.
Msimu uliopita, Swansea ilishinda 2-0
Stamford Bridge katika Mechi ya Nusu Fainali ya Capital One Cup.
Hali za Wachezaji
Huku akikabiliwa na Mechi ngumu
Jumamosi dhidi ya Liverpool, Jose Mourinho huenda akabadili Kikosi chake na
kuwapumzisha baadhi ya nguzo zake akiwemo Nahodha John Terry.
Meneja wa Swansea, Michael Laudrup,
atawakosa Majeruhi Michu, Nathan Dyer na Michel Vorm.
Vikosi vitatokana na:
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cole, Luiz, Essien, Ramires, Lampard,
Torres, Mata, Oscar, Mikel, Schurrle, De Bruyne, Hazard, Ba, Willian,
Schwarzer, Cahill, Terry, Azpilicueta, Eto'o, Blackman, Bertrand.
Swansea: Amat, Taylor, Flores, Williams, Britton, Shelvey, Bony,
Hernandez, Lamah, Routledge, Tiendalli, De Guzman, Canas, Pozuelo, Tremmel,
Vazquez, Richards, Davies, Zabret.
Everton Vs Sunderland
Mchezaji wa Mkopo kutoka Chelsea,
Romelu Lukaku, ndie mashine ya Magoli kwa Everton na ana Rekodi nzuri dhidi ya
Sunderland kwa kuifunga Bao 3 katika Mechi mbili za Ligi akicheza dhidi yao.
Mwezi Aprili, Sunderland iliifunga
Everton na na kumaliza ukame wa Mechi 16 za kutoifunga Everton ambazo walipata
Sare 4 na Kufungwa 12 katika hizo.
Hali za Wachezaji
Everton inacho Kikosi kamili lakini
Sunderland itawakosa Wes Brown, Kifungoni Mechi 3 baada Kadi Nyekundu
walipocheza na Norwich Mechi iliyopita, na pia Majeruhi Kipa Keiren Westwood na
Beki Carlos Cuellar.
Vikosi vitatokana na:
Everton: Howard, Robles, Coleman, Hibbert, Distin, Jagielka, Oviedo,
Stones, Heitinga, Alcaraz, Baines, Mirallas, Barry, McCarthy, Pienaar, Barkley,
Osman, Naismith, Lukaku, Vellios, Jelavic.
Sunderland: Mannone, Pickford, Celustka, Dossena, Bardsley, O'Shea,
Diakite, Roberge, Cattermole, Cabral, Gardner, Ki, Giaccherini, Johnson,
Larsson, Ba, Karlsson, Mavrias, Fletcher, Altidore, Borini.
Newcastle Vs Stoke City
Yohann Cabaye na Papiss Demba Cisse,
wote wameifungia Newcastle Bao 3 katika Mechi 3 za Ligi dhidi ya Stoke
City.
Nae Jon Walters wa Stoke amefunga Bao
katika Mechi 4 kati ya 5 walizocheza na Newcastle.
Hali za Wachezaji
Bosi wa Newcastle Alan Pardew atamkosa
Kiungo kutoka Ivory Coast Cheick Tiote ambae yupo Kifungoni Mechi 1 baada
kukusanya Kadi za Njano 5.
Nae Bosi wa Stoke Mark Hughes anao
uamuzi wa kumuanzisha Charlie Adam baada kucheza vizuri Mechi iliyopita
akitokea Benchi na kufunga Bao lakini atamkosa Beki
Robert Huth ambae amefanyiwa operesheni
ya Goti.
Vikosi vitatokana na:
Newcastle: Krul, Elliot, Debuchy, Coloccini, Williamson, Yanga-Mbiwa,
S. Taylor, Santon, Dummett, Haidara, Anita, Cabaye, Marveaux, Sissoko, Ben
Arfa, Gutierrez, Sammy Ameobi, Bigirimana, Obertan, Cisse, Remy, Gouffran,
Shola Ameobi.
Stoke: Sorensen, Begovic, Cameron, Wilson, Shawcross, Muniesa,
Wilkinson, Palacios, Pennant, Nzonzi, Walters, Assaidi, Ireland, Crouch, Jones,
Pieters, Arnautovic, Adam, Shea, Whelan.
Norwich Vs Fulham
Ingawa Norwich City wamefungwa Mechi 3
tu kati ya 17 za Ligi walizocheza Nyumbani kwa Mwaka 2013 wakiwa Wameshinda 6
na Sare 8, Msimu huu hawafanyi vizuri sana kwenye Ligi lakini hii ni nafasi
kwao kwani hata Fulham wana matatizo makubwa.
Hali za Wachezaji
Norwich hawana matatizo kwenye
Wachezaji wao lakini Fulham huenda wakamkosa tena Straika wao Dimitar Berbatov
ambae aliikosa Mechi iliyopita waliyofungwa 4-2 na Manchester City kwa kuwa na
tatizo la Nyonga.
Vikosi vitatokana na:
Norwich: Ruddy, Whittaker, Bassong, Turner, Olsson, Johnson, Fer,
Howson, Redmond, Hoolahan, Hooper, Bunn, Josh Murphy, Becchio, Elmander,
Garrido, R Bennett, Martin, Snodgrass, van Wolfswinkel, Nash.
Fulham: Stekelenburg, Riether, Hughes, Riise, Sidwell, Parker, Karagounis,
Dejagah, Berbatov, Kacaniklic, Kasami, Ruiz, Bent, Stockdale, Richardson, Duff,
Zverotic, Vigen Christensen, Amorebieta.
Tottenham Vs West Bromwich
Tottenham wanatinga kwenye Mechi hii
ikiwa ni Mechi ya kwanza tangu Meneja wao wa muda Tim Sherwood
kuthibitishwa kwenye wadhifa aliouchukua Wiki iliyopita baada kutimuliwa Andre
Villas-Boas.
Hii ni Mechi ambayo Tottenham wana
Rekodi nzuri dhidi ya West Brom kwa kutofungwa katika Mechi 7 walizocheza mwisho
nao wakiwa wametoka Sare 3 na Kushinda 4 huku Straika wao Jermain Defoe
akifunga katika Mechi 3 kati ya hizo.
Hali za Wachezaji
Tottenham itawakosa Majeruhi Andros
Townsend, Younes Kaboul na Jan Vertonghen wakati Paulinho yupo Kifungoni.
West Brom wana Kikosi kamili ukiondoa
Straika Victor Anichebe ambae uhakika wa kucheza kwake utaamuliwa Dakika za
mwisho kwa vile ana maumivu kidogo.
Vikosi vitatokana na:
Tottenham: Lloris, Friedel, Walker, Naughton, Rose, Fryers, Dawson,
Chiriches, Capoue, Dembele, Sigurdsson, Eriksen, Chadli, Bentaleb, Fredericks,
Lamela, Holtby, Adebayor, Defoe, Soldado.
West Bromwich: Foster, Myhill, Daniels, Jones, Ridgewell, Olsson, McAuley,
Lugano, Brunt, Sessegnon, Amalfitano, Mulumbu, Berahino, Yacob, Anichebe,
Vydra, Long, Anelka, Morrison, Popov, Dawson, Reid, Sinclair, Gera, Rosenberg.
West Ham Vs Arsenal
Katika Mechi 10 za mwisho za Ligi, West
Ham wamefungwa Mechi 8 na Sare 2.
Hali za Wachezaji
Nahodha wa West Ham, Kevin Nolan,
atarejea Kikosini baada kukamilisha Kifungo chake lakini Majeruhi Andy Carroll,
Ricardo Vaz Te na Winston Reid hawatakuwepo.
Arsenal itamkosa Jack Wilshere ambae
ndio atakuwa akikamilisha Kifungo cha Mechi mbili.
Sentahafu Laurent Koscielny na Lukas
Podolski wanaweza kurudi baada kupona lakini Yaya Sanogo, Alex
Oxlade-Chamberlain na Abou Diaby bado wako nje wakiwa wana maumivu.
Vikosi vitatokana na:
West Ham: Adrian, Demel, Tomkins, Collins, McCarthy, Noble, Diame,
Nolan, Morrison, Jarvis, Maiga, Rat, Collison, O'Brien, Diarra, Jaaskelainen, C
Cole, J Cole.
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Vermaelen, Gibbs, Flamini,
Arteta, Ramsey, Ozil, Walcott, Giroud, Fabianski, Monreal, Bendtner, Cazorla,
Rosicky, Arteta, Jenkinson, Podolski, Gnabry, Koscielny.
*BIG MATCH* MANCHESTER CITY Vs LIVERPOOL
Kwa Mechi za Nyumbani 8 za Ligi za
Msimu huu, Man City wameshinda zote na kufunga Jumla ya Mabao 35 na Timu
pekee iliyowahi kufunga Bao kama hizo kwenye Mechi za kwanza za Ligi 8 ni Spurs
katika Msimu wa 1962/3.
Mechi 6 kati ya 9 za Ligi Kuu England
kati ya Liverpool na Man City zimekuwa Sare nyingine zikiwa City Kushinda 2 na
Liverpool 1.
Liverpool wanaingia kwenye Mechi hii
wakiwa wameshinda Mechi 1 tu ya Ugenini katika 5 walizocheza mwisho huku
nyingine zikiwa Sare 2 na Kufungwa 2.
Hali za Wachezaji
Kipa wa Manchester City Joe Hart
anatarajiwa kubaki Golini baada kubwagwa nje kwa muda mrefu na kurejeshwa
Kikosini Mechi iliyopita walipoifunga Fulham 4-2.
City itawakosa Majeruhi Pablo Zabaleta,
Micah Richards, Sergio Aguero na Matija Nastasic wakati Stevan Jovetic akiwa
bado ni Mgonjwa.
Liverpool huenda ikamkosa Fulbeki Jon
Flanagan baada kupata maumivu katika Mechi ya Jumamosi iliyopita walipoifunga
Cardiff.
Majeruhi wa Liverpool ambao hawatacheza
ni Nahodha Steven Gerrard, Daniel Sturridge na Jose Enrique.
Hali hii imemlazimisha Meneja wa
Liverpool, Brendan Rodgers, kuchomekea Wachezaji toka Timu ya Rizevu kwani
Kikosi cha Kwanza kimebakiwa na Wachezaji 17 tu ambao ni fiti.
Vikosi vitatokana na:
Man City: Pantilimon, Hart, Boyata, Milner, Kompany, Demichelis,
Lescott, Clichy, Kolarov, Nasri, Silva, Navas, Garcia, Fernandinho, Toure,
Rodwell, Dzeko, Negredo, Guidetti, Jovetic.
Liverpool: Mignolet, Johnson, Skrtel, Sakho, Agger, Flanagan, Lucas,
Henderson, Allen, Sterling, Coutinho, Suarez, Jones, Kelly, Toure, Alberto,
Aspas, Moses, Cissokho.
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Desemba 28
1545 West Ham v West Brom
1800 Aston Villa v Swansea
1800 Hull v Fulham
1800 Man City v Crystal Palace
1800 Norwich v Man United
2030 Cardiff v Sunderland
Jumapili Desemba 29
1630 Everton v Southampton
1630 Newcastle v Arsenal
1900 Chelsea v Liverpool
1900 Tottenham v Stoke
Jumatano Januari 1
1545 Swansea v Man City
1800 Arsenal v Cardiff
1800 Crystal Palace v Norwich
1800 Fulham v West Ham
1800 Liverpool v Hull
1800 Southampton v Chelsea
1800 Stoke v Everton
1800 Sunderland v Aston Villa
1800 West Brom v Newcastle
2030 Man United v Tottenham
++++++++++++++++++++++++++++++++
LIGI KUU ENGLAND:
MSIMAMO:
|
NA
|
TIMU
|
P
|
GD
|
PTS
|
|
1
|
Liverpool
|
17
|
23
|
36
|
|
2
|
Arsenal
|
17
|
16
|
36
|
|
3
|
Man City
|
17
|
31
|
35
|
|
4
|
Chelsea
|
17
|
14
|
34
|
|
5
|
Everton
|
17
|
13
|
34
|
|
6
|
Newcastle
|
17
|
2
|
30
|
|
7
|
Tottenham
|
17
|
-5
|
30
|
|
8
|
Man United
|
17
|
8
|
28
|
|
9
|
Southampton
|
17
|
4
|
24
|
|
10
|
Stoke
|
17
|
-4
|
21
|
|
11
|
Swansea
|
17
|
0
|
20
|
|
12
|
Hull
|
17
|
-6
|
20
|
|
13
|
Aston Villa
|
17
|
-6
|
19
|
|
14
|
Norwich
|
17
|
-14
|
19
|
|
15
|
Cardiff
|
17
|
-12
|
17
|
|
16
|
West Brom
|
17
|
-5
|
16
|
|
17
|
West Ham
|
17
|
-8
|
14
|
|
18
|
Crystal Palace
|
17
|
-16
|
13
|
|
19
|
Fulham
|
17
|
-17
|
13
|
|
20
|
Sunderland
|
17
|
-18
|
10
|

No comments:
Post a Comment