![]() |
| Marehemu Clement Mabina |
MAZISHI ya
aliyekuwa mwenyekiti wa CCM na Diwani wa Kata ya Kisesa wilayani Magu Clement
Mabina, aliyeuawa kikatili na kundi la wananchi, yanatarajiwa kufanyika
Alhamisi.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa
familia ya marehemu Mabina, Timothy Gregory ambaye ni mdogo wa marehemu,
alisema kwamba, mipango ya mazishi imekamilika na zaidi ni pamoja na kusubilia
mtoto wa kike wa marehemu aliyoko njiani kutokea nchini Uingereza marehemu
waliokuwa nje ya nchi.
Gregory alisema, Kijana mdogo wa
marehemu (mtoto ) tayari amewasili jana jioni, hivyo mazishi marehemu Mabina
yatafanyika kesho kutwa Kisesa wilayani Magu baada ya mtoto wake mkubwa wa kike
kuwasili kutoka Uingereza.
Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi
hayo, Henry Matata ambaye ni Meya wa Manispaa ya Ilemela, amesema kuwa,
taratibu za maziko ya marehemu Mabina, zinaendelea kufanyika nyumbani kwa
marehemu na kupokea wageni mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, wanasiasa wa
Kada mbalimbali kutoka vyama vya siasa na serikali pamoja na ndugu na rafiki wa
karibu na marehemu wa sehemu tofauti nchini kote na nje ya nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
![]() |
| Marehemu Clement Mabina (Kushoto)akiwa na Rais Jakaya Kikwete(katikati) |
“Marehemu Mabina atazikwa rasmi
Alhamisi saa 7:00 mchana katika shamba lake kulekule Kitongoji cha Kanyama
alikouawa. Tayari tumerudisha mabango ya kuzuia watu waliokuwa wakichimba mawe
na mchanga kwenye eneo hilo, yaliyoondolewa na kundi la watu waliomshambulia na
majirani wamepokea na kudai eneo hilo lilikuwa likimilikiwa na marehemu
kihalali kwani serikali ya kijiji ililikabidhi kwa marehemu kupitia mkutano wa
hadhara hali iliyodaiwa kumuua ilikuwa kumuonea na ilitawaliwa na siasa zaidi
kuliko uhalisia wa madai ya kundi la watu hao wachache .” alidai Matata.
Hadi sasa, mamia ya waombolezaji
wakiwemo ndugu, jamaa, wananchi wa Kisesa, wana CCM na viongozi mbalimbali wa
Chama na serikali walikuwa wakiendelea kumiminika nyumbani hapo kuomboleza.
Nacho Chama Cha Mapinduzi (CCM)
mkoani Mwanza, Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mwanza, Anthony
Diallo kimetoa pole kwa wananchi wa Kisesa wakiwemo ndugu na jamaa
wa familia za marehemu Mabina na mtoto Temeli Malimi (12)
aliyeuawa kwa kupigwa risasi na marehemu huyo wakati wa purukushani
za kujiokoa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya
ya Magu, Desidery Kiswaga alisema kwamba, marehemu Mabina aliyekuwa Mweneykiti
wa zamani wa CCM mkoa wa Mwanza, atazikwa kwa heshima zote stahili.
![]() |
| Hivi ndivyo alivyo uwawa |



No comments:
Post a Comment