HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 21 November 2013

WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI MKOANI IRINGA WAPORWA SH MIL 8 NA MAJAMBAZI




IRINGA
WATU wanne wasiofahamika wamewavamia wachimbaji wadogo wadogo wa madini aina ya dhahabu na kuwapora sh milioni nane.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Nyegesa Wankyo, alisema watu hao walivamia machimbo hayo yaliopo Ihanzutwa, Tarafa ya Sadani, Wilaya ya Mufindi, juzi majira ya saa 3 usiku wakiwa na gari aina ya GX 100 nyeusi ambayo haikutambulika namba zake.
Wankyo alisema watu hao walipofika walifyatua risasi hewani na kisha kuanza kupora fedha hizo na simu za mkononi.
Alisema Jeshi la Polisi mkoani hapa linaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Katika tukio jingine, Hubiri Vaiga (32) ameuawa kwa kuchomwa na kisu sehemu ya ubavuni na Nisa Fodi (20).
Kamanda Wakyo alisema tukio hilo lilitokea juzi, saa 4 usiku katika Kitongoji cha Mwingila, Kijiji cha Mbawi Masisiwe, Wilaya ya Kilolo. Chanzo cha ugomvi ni ulevi, na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi.

No comments:

Post a Comment