
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWAVYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
na Usalama Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, amewapandisha vyeo maafisa 77 wa
Jeshi la Polisi kutoka cheo cha Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).
Miongoni mwa
maafisa waliopandishwa vyeo kutoka cheo cha Kamishina Msaidizi wa Polisi kuwa
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ni pamoja na Mkuu wa Upelelezi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishina msaidizi wa Polisi ACP Ahmed Msangi,
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Temeke Kamishina Msaidizi wa Polisi
(ACP) Engelbert Kiondo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala ACP. Marietha
Minangi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya ACP. Diwani Athumani na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Singida Geofrey Kamwela.
Wengine ni Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kigoma ACP. Frasser Kashai, Kamanda wa Polisi mkoa wa
Morogoro ACP. Faustine Shilogile, Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma ACP. David
Misime, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara ACP. Ferdinand Mtui, Kamanda wa Polisi
mkoa wa Tanga ACP.
Costantine Massawe,
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita ACP. Leornad Paul, Kamanda wa Polisi mkoa
wa Pwani ACP. Ulrich Matei na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi ACP. George
Mwakajinga.
Zaidi ya hao
wengine ni, Kamanada wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP. Evarist Mangala, Kamanda
wa Polisi mkoa wa Ruvuma Deusedit Nsimeke, Kamanada wa Polisi mkoa wa
Njombe ACP. Fulugence Ngonjani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari na baadhi ya Makamanda wa vikosi, Wakuu wa vitengo, Mkuu wa
Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi na Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar Es
salaam.
Kufuatia
kupandishwa vyeo kwa Maafisa hao wa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini IGP Said Mwema, amemshukuru Rais wa Jamuhuru ya Muungano wa Tanzania na
Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mhe. Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete kwa kutambua mchango wa Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi
na usalama wa raia na mali zao.
Aidha, IGP Mwema
amewapongeza wale wote waliopandishwa vyeo, na kuwataka kuendelea kufanya kazi
kwa juhudi na weledi katika kuimarisha Usalama wa raia na mali zao kwa kuwa
cheo ni dhamana.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la
Polisi.
No comments:
Post a Comment