| Mtoto Jacline Staniely[9] baada ya kupatiwa Matibabu |
| Picha ya X-Ray ikionesha kidole cha kati kilicho vunjika |
Wiki ya kupinga vitendo vya ukatili wa
kijinsia na watoto ikiwa imeanza kuadhimishwa duniani Novemba 25 mwaka huu bado
vitendo hivyo vimezidi kushamiri Mkoani Mbeya ambapo mwanafunzi wa darasa la
nne shule ya msingi Aiport Kata ya Iyela jijini Jacline Staniely[9] kuumizwa
mkono wake wa kushoto.
Jacline akiongea kwa ridhaa ya mama
yake amesema alipigwa kwa kutumia ubao na mwalimu wa shule hiyo Novemba 19
mwaka huu na mwalimu Kanyika kwa kosa la kuwa na nywele ndefu.
Mwanafunzi huyo amedai kuwa siku ya
tukio alipigwa vibaya na kumsababishia maumivu makali ambapo siku hiyo mama
yake alikuwa safarini Nairobi Kenya hivyo hakupata matibabu ambapo alilazimika
kumwambia mwalimu jirani[Bibi]ambaye alimpeleka hospitali kutibiwa.
Hata hivyo Jackline amesema kuwa
kutokana na maumivu makali alilazimika kufanya mtihani wa Taifa wa darasa la
nne bila kupata matibabu ya kutosha.
Baada ya kurejea kutoka safari mama
yake mzazi aitwae Rehema Adamson Ndeje[28] mkazi wa Block T jijini Mbeya amesema
baada ya maumivu ya mwanae usiku ilimlazimu kwenda shuleni ili kujua
kulikoni,ndipo alipoonana na mwalimu Kanyika baada ya kukutanishwa na Mwalimu
mkuu.
Mama Jackine amesema hicho ni kipigo
cha tatu kukubwa kwa mwanae kupigwa na mwalimu huyo ambapo alionesha makovu
yaliyodaiwa yalitokana na vipigo vya mwalimu huyo miguuni akidai majeraha hayo
yalidumu kwa miezi mitatu.
Hata hivyo Rehema aliamua kwenda Polisi
Mwanjelwa kutoa taarifa za tukio na kila alipoitwa mwalimu huyo hakutokea ndipo
jalada likapelekwa kituo kikuu cha kati ambapo mwalimu alikamatwa na mhanga
kupewa PF 3 kwa ajili ya matibabu ambapo alipigwa picha na kuonekana moja ya
kidole cha kati cha kushoto kuoneka kuathirika kutokana na kupigwa kwa kutumia
ubao.
Mzazi huyo amesema hana ni mbaya na
mwalimu Kanyika lakini kitendo cha kumwadhibu mwanae mara kwa mara ndicho
kimemtia shaka hata kuamua kutoa taarifa Polisi ili sheria ichukue mkondo wake.
Mwandishi wa habari hii alipofika
shuleni ili kujua mustakabali wa suala hili mwalimu alitoa nje mwandishi akidai
yeye ana majukumu mengine lakini baada ya kufuatilia mkuu huyo alichukua gari
lake aina ya RAV 4 na kwenda nyumbani kwa Mzazi wa mtoto na kwenda naye
hospitali akiwa ameambatana na mmoja wa walimu wa shule hiyo ambaye ni jirani
ambapo Jackline humwita Bibi.
Mwandishi alimtafuta mmoja wa
wanaharakati wa kijinsia ambaye alikiri kupokea lalamiko hilo ingawa alijibu
kwa mkato kuwa mtoto huyo kaumia kidogo tu na ni usanii mtoto huyo kufungwa POP
na kwamba bado PF3 haijajazwa kitu hivyo hawezi kuzungumzia lolote.
Kumekuwa na malamiko mengi katika
Dawati hilo kutokana na matukio kutochunguzwa kwa wakati hali inayotoa mwanya
kwa vitendo hivyo kuibuka mara kwa mara na wahalifu kutoroka mkono wa sheria
lakini baadhi kuwa na utendaji duni licha ya taarifa kutolewa kwa wakati.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya ameahidi
kulifuatilia suala hilo na ikibainika mtuhumiwea atafikishwa mahakamani ili
kujibu tuhuma zinazomkabili.
Na Ezekiel Kamanga
Mbeya yetu
No comments:
Post a Comment