DIWANI wa Viti Maalumu Kata ya
Chumbageni jijini Tanga kupitia chama
cha Mapinduzi (CCM)Saida Gadafi amelishauri baraza la madiwani kuridhia
soko la kuuzia samaki la deepsea livunjwe kuliko kila mwaka litengewe
sh.milioni 50 kwa ajili ya ukarabati wake.
| Samaki wakiandaliwa kwa ajili ya kuuzwa |
Gadafi alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika katika ukumbi wa mipango miji jijini Tanga ambapo alisema fedha
hizo zinazotengwa hazionekani zinafanyia kazi gani kwa sababu ukarabati wenyewe
hauonekani kama umefanyika.
Alisema kitendo hicho kinapelekea
kurudisha nyuma kasi ya maendeleo ya halmashauri hiyo na kueleza kwa maslahi
yake inabidi soko hilo livunjwe lakini mchakato huo uendane na kuwashirikisha
wataalamu ili waweze kuamua nini kifanyike.
| Samaki wakiwa Mezani kwa Mauzo |
Diwani huyo alisema lazima madiwani
wahakikishe wanakuwa mstari wa mbele kusimamia maslahi ya wananchi
wanaowaongoza ili kuondoa kero zao lengo likiwa ni kuwapa maendeleo.
“Kila mwaka zilikuwa zikitengwa milioni 50 kwa ajili ya ukarabati wa
soko hilo lakini watu walikuwa hawazisema ila hizo milioni 11 kwa ajili ya
kupewa mtathimini zimekuwa zikileta maneno naamini wataalamu tunao kwenye
halmashauri waamue nini cha kufanya pale lakini hilo soko bora livunjwe “Alisema
Gadafi.
![]() |
| Hivi ndivyo samaki wanavyouzwa katika soko hilo |
Akizungumza suala hilo,Mjumbe wa
Kamati wa Fedha,Shehe Fadhili Bwanga alisema masuala ya kuvunjwa soko hilo ni
kutokana na kuona kuwa halikidhi haja ya kuendana na hadhi ya jiji na wao
kupitia kamati ya fedha wameona zifuatwe sheria za nchi ikiwemo kuthaminiwa na
kampuni zinazotambulika kiserikali ili ziweze kutoa idhini ya uvunjwaji wa
jengo hilo.
Bwanga aliongeza kuwa uamuzi wa
kuvunja soko hilo pia utatokana na gharama zake za sh.milioni 11 lakini sheria
za uvunjwaji zilizowekwa inabidi zifuatwe kabla ya kuachukua maamuzi wa
uvunjwaje wake.

No comments:
Post a Comment