HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Monday, 4 November 2013

KIGOGO WA NCCR-MAGEUZI ASHAMBULIWA





Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengodo Mvungi akitolewa na wauguzi kutoka chumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI) na kupelekwa Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa vipimo jana.

Dar es Salaam. 
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini, Dk Sengondo Mvungi amejeruhiwa usiku wa kuamkia jana, baada ya kukatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana waliovamia nyumbani kwake Mpiji-Magohe, jijini Dar es Salaam.

Dk Mvungi, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi aliwahishwa kwenye Taasisi ya Mifupa Hospitali ya Muhimbili (MOI), ambako amelazwa katika wodi maalumu huku hali yake ikiwa mbaya.

Taarifa kutoka kwa ndugu na watu waliomtembelea hospitalini hapo wanasema kwamba hali ya Dk Mvungi ni mbaya kwani alikuwa hawezi hata kuzungumza.
Akisimulia tukio hilo, dereva wa Dk Mvungi anayeitwa Emmanuel Ntaro, alisema akiwa nyumbani kwake majira ya saa 6:30 usiku, alisikia mlipuko mkubwa kisha zikasikika kelele zikitokea nyumbani kwa bosi wake.

“Nilifika na kukuta hajitambui, tukampeleka Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani alikopatiwa huduma ya kwanza kabla ya kumpeleka MOI ambako anaendelea kuchunguzwa na kupatiwa matibabu,” alieleza Ntaro

Alisema kuwa watu wapatao sita, walivamia nyumbani kwa Dk Mvungi ambako baada ya kuvunja mlango na kuingia ndani, walimjeruhi kwa kutumia mapanga huku wakidai wapatiwe fedha. Watu hao walimsababishia majeraha usoni, kichwani na sehemu nyingine za mwili.
Akizungumza na Wanahabari  jana, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia alisema mbali na kupata matibabu MOI, pia walilazimika kumpeleka Hospitali ya Aga Khan kwa ajili ya vipimo zaidi katika mashine ya CT Scan kama walivyoshauriwa na madaktari wa zamu.

Mbatia alisema kuwa baada ya Dk Mvungi kufanyiwa kipimo hicho alirudishwa tena MOI kwa matibabu na uangalizi maalumu. “Hali yake inaanza kuimarika tofauti na nilivyomuona saa nne asubuhi, “ alisema Mbatia muda wa saa 12 jioni jana alipozungumza na wanahabari jijini Dar.
Alisema kwamba pia watu waliohusika na tukio hilo waliiba kompyuta mpakato (laptop) pamoja na bastola ya Dk Mvungi.

Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni, Cammilius Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Kweli hilo ni tukio la kihalifu na sisi tunaendelea kulifanyia kazi. Tunawahakikishia Watanzania kuwa watu hao watapatikana na kufikishwa kwenye mkono wa kisheria,” alisema.

No comments:

Post a Comment