HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Monday, 18 November 2013

*HATARI* UTAFITI WAONESHA KUWA KARIBU NUSU YA MADAKTARI WAMEACHA KUTIBU


Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Husein Mwinyi


Dar es Salaam.
Imebainika kuwa asilimia 39.6 ya madaktari wenye shahada nchini hawafanyi kazi ya kutoa huduma ya kitabibu wala za kiutawala katika sekta ya afya na badala yake kufanya shughuli nyingine tofauti kabisa na masuala waliyosomea.
Utafiti uliofanywa na Chama cha Madaktari Tanzania (Mat) kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la Sikika, umebaini pia kwamba kati ya asilimia 60 iliyobaki, ni asilimia 42.9 tu wanaofanya kazi ya kutoa huduma za kitabibu moja kwa moja na wengine ama wapo masomoni, wanafanya kazi katika mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO), taasisi zinazojishughulisha na utafiti na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika, Irenei Kiria alisema utafiti huo uliojumuisha madaktari 2,246 wa Kitanzania waliosambaa sehemu mbalimbali duniani, asilimia 32 ya madaktari hao wanaofanya kazi wapo Dar es Salaam, asilimia tano wapo Mwanza, asilimia 2.3 Kilimanjaro, asilimia 2.1 Mbeya huku asilimia 8.2 (madaktari 184) wakifanya kazi nje ya nchi. Madaktari wengi wapo Uganda (38) na Amerika Kaskazini (38), Ulaya (27) na Afrika Kusini (12). Aidha, utafiti huo umebaini kwamba asilimia 38.8 ya madaktari waliohojiwa hawakuwa na vituo vya kazi.
Kiria alisema tatizo la madaktari wanaohitimu kutokufanya kazi zinazoendana na taaluma hiyo ni kubwa akitolea mfano wa wahitimu 107 wa shahada ya udaktari mwaka 2003 ambao alisema 48 kati yao hawafanyi kazi ya utabibu.
“Madaktari 68 kati ya 102 ambao ni sawa na theluthi mbili ya wahitimu wa mwaka 2004 na zaidi ya robo tatu ya (176 kati ya 224) ya wahitimu wa mwaka 2008 na wahitimu 155 kati ya 206 ya wahitimu wa mwaka 2009 ndiyo wanaofanya kazi ya utabibu,” alisema.

Athari za tatizo
Kiria alisema kutokana na kukimbiwa huko kwa taaluma, daktari mmoja wa Tanzania hivi sasa analazimika kutibu wagonjwa 30,000 badala ya kiwango cha daktari mmoja wagonjwa 10,000 kilichopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
“Lakini mbali na hilo, kwa kuwa madaktari wengi wapo Dar es Salaam, wagonjwa katika mikoa mingine wamekuwa wakiwafuata na hivyo kuwafanya kuwa na mzigo mkubwa wa kutoa huduma ambazo zingeweza kumalizwa katika maeneo yao. Upo umuhimu mkubwa wa kuhakikisha kunakuwa na mgawanyo wa madaktari.”
Rais wa Mat, Dk Primus Saidia alisema kitendo cha madaktari hao kuachana na taaluma hiyo, licha ya kuwa na athari kubwa kiuchumi, kinalitia hasara taifa akisema kusomesha daktari mmoja mpaka kuhitimu hugharimu wastani wa Dola za Marekani 40,000 mpaka 60,000 (Sh62 milioni mpaka Sh94 milioni).
Alisema tatizo hilo la upungufu wa madaktari ni la siku nyingi akitoa mfano wa utafiti uliofanywa na Sikika mwaka 2011 ambao ulionyesha kwamba wilaya 30 nchini hazikuwa na madaktari wenye shahada.
Alisema chama chake kitafanya mkutano wake mkuu Novemba 28, mwaka huu ambao pamoja na mambo mengine, utajadili kwa kina tatizo hilo na kutoa mapendekezo yake kwa Serikali na wadau wengine.
Credit: Mwananchi

No comments:

Post a Comment