Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) umeingia katika
mvutano mkubwa na Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kuhusu Mkutano Mkuu
Maalum wa chama hicho tawala uliopangwa kufanyika Julai 23 mwaka huu mjini
Dodoma.
UVCCM
wameionya BAVICHA kuhusu mpango wao wa kutaka kukusanyika mjini Dodoma siku
hiyo kwa lengo la kuzuia mkutano huo kwa madai kuwa unakiuka amri halali ya
polisi ya kupiga marufuku kufanyika kwa mikutano yote ya kisiasa nchini.
Onyo
hiyo limetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamda Shaka ambaye
aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa watawakabili kwa
nguvu zote BAVICHA endapo wataamua kuendesha siasa zinazolenga kuvuruga amani
na kuleta hofu katika jamii na kutishia maisha.
Alisema
umoja huo hautaona shaka kutumia mbinu zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau miongo
kadhaa iliyopita nchini Kenya.
“Hatutaona
muhali kupita njia zilizotumiwa na wapiganaji wa Maumau wa Kenya ili kukihami
chama, kulinda viongozi wake na kupigania hadhi na heshima yetu,” alisema Kaimu Katibu Mkuu
huyo wa UVCCM.
CCM
inatarajia kufanya mkutano mkuu maalum Julai 23 mwaka huu ambapo Rais John
Magufuli atakabidhiwa rasmi uenyekiti wa chama hicho kutoka kwa mtangulizi
wake, Dk. Jakaya Kikwete.
No comments:
Post a Comment