Wakati jeshi la polisi likisema linajiimarisha,
vitendo vya ujambazi vinazidi kuitikisa nchi baada ya kundi la watu
wasiojulikana kuvamia ofisi za Kampuni ya Ahsante Tours ya mjini Moshi, kuua
walinzi wawili na kuiba Sh 65.5milioni.
Tukio
hilo limekuja siku chache baada ya watu wasiojulikana kuvunja duka la
kubadilisha fedha la Chase Forex Bureau De Change la mjini Moshi na kuiba zaidi
ya Sh120 milioni.
Mbali
na tukio hilo, Juni 12 mwaka huu, watu watano wakiwa na bunduki aina ya SMG,
walivamia mji wa Magugu wilayani Babati mkoani Manyara na kupora Sh2.5
milioni.
Tofauti
na tukio hilo la Magugu, hivi karibuni Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
waliwaua watu watatu eneo la Masaki katika majibizano ya risasi na
Polisi.
Ukiachilia
matukio hayo, taarifa kutoka mikoa mbalimbali nchini zinaonyesha uporaji wa
fedha na mali kwa kutumia pikipiki maarufu kama bodaboda, unazidi kushika kasi
maeneo mbalimbali.
Wengi
wa wanaolengwa na wahalifu hao ni wateja wanaotoka kuchukua pesa benki au
wanaokwenda kuchukua fedha jambo ambalo limezua hofu kuwa huenda baadhi ya
wafanyakazi wa benki wanashirikiana na wahalifu.
Lakini,
tishio kubwa zaidi la uhalifu linatokana na kuibuka kwa makundi ya kihalifu
yanayokuwa yamejihami kwa silaha za kivita, yakiwamo mabomu ya kurushwa kwa
mkono, yakichinja raia na kupora.
Hivi
karibuni, Polisi Jijini Dar es Salaam waliwaua watuhumiwa hatari wawili
waliokuwa wamejihami kwa bunduki na mabomu, wanaotuhumiwa kuchinja watu nane
Jijini Tanga na watatu Jijini Mwanza
Hali hii ndio imemsukuma Rais John Pombe Magufuli, kuwaagiza polisi kuhakikisha ‘wanawanyang’anya’ majambazi silaha haraka kabla ya kuwadhuru polisi ama raia wasio na hatia.
Hali hii ndio imemsukuma Rais John Pombe Magufuli, kuwaagiza polisi kuhakikisha ‘wanawanyang’anya’ majambazi silaha haraka kabla ya kuwadhuru polisi ama raia wasio na hatia.
Uporaji
Ahsante Tours
Tukio la mauaji ya walinzi wawili ofisi za Ahsante Tours, lilitokea usiku wa kuamkia jana, baada ya watu hao kuwazidi nguvu walinzi na kuwafunga kamba kisha kuwapiga kwa kitu butu kichwani.
Tukio la mauaji ya walinzi wawili ofisi za Ahsante Tours, lilitokea usiku wa kuamkia jana, baada ya watu hao kuwazidi nguvu walinzi na kuwafunga kamba kisha kuwapiga kwa kitu butu kichwani.
Kampuni
hiyo inamilikiwa na mfanyabiashara Cathbert Swai na mkewe Stella Shangali, ambao
pia wanamiliki hoteli ya kitalii ya Weruweru River Lodge iliyopo Mailisita, nje
kidogo ya mji wa Moshi.
Taarifa
kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ambayo ni moja kati ya kampuni
zinazoongoza kwa kupokea watalii wengi, zinadai huenda tukio hilo ni mpango wa
ndani.
“Kuna
maswali mengi tunajiuliza. Walijuaje kuna kiasi hicho kikubwa cha fedha kama
taarifa hazikutoka miongoni mwetu?” alihoji mmoja wa wafanyakazi aliyeomba jina
lake lisitajwe.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa, alisema kati ya fedha
zilizoibwa, kulikuwa na Dola za Marekani (Sh50 milioni) na Sh15 milioni
za Tanzania.
Walinzi
waliouawa wametajwa kuwa ni Omar Mohamed (48), mkazi wa Matindigani Pasua na
Dominick Cheddy (41), mkazi wa Mailisita na wote ni wenyeji wa mkoa wa
Tanga.
Kamanda
Mutafungwa alisema tukio hilo liligunduliwa saa 1.00 asubuhi na wasamaria wema
waliotoa taarifa polisi, na uchunguzi wa awali umebaini watu hao walikata uzio
wa ofisi hizo.
“Baada
ya kuingia ndani ya jengo hilo la ofisi walivunja ofisi ya meneja mkuu na
baadaye ofisi ya mhasibu ndio wakaiba Dola 23,300 na pesa za Tanzania Sh15
milioni,”alisema
Kamanda Mutafungwa.
“Tunashuku
kuwa huenda hao majambazi waliamua kuwaua hao walinzi baada ya hao walinzi kuwatambua.
Bahati mbaya hawakuwa na silaha yoyote hata panga hawakuwa nalo,”alisisitiza.
Kamanda Mutafungwa alisema Polisi inamshikilia mtu mmoja ambaye inaonekana alikuwepo wakati mauaji na uporaji huo ukifanyika lakini, majambazi hao hawakumdhuru sehemu yoyote.
Kamanda Mutafungwa alisema Polisi inamshikilia mtu mmoja ambaye inaonekana alikuwepo wakati mauaji na uporaji huo ukifanyika lakini, majambazi hao hawakumdhuru sehemu yoyote.
Hata
hivyo, Kamanda Mutafungwa, aliwataka wafanyabiashara kupeleka pesa benki badala
ya kuzihifadhi ndani au ofisini na kuwataka pia kuimarisha ulinzi ikiwamo
kuweka CCCTV Camera.
Alitoa
wito kwa wananchi wenye taarifa za waliohusika na tukio hilo, kulisaidia Jeshi
la Polisi kama ilivyotokea wiki moja iliyopita ambapo taarifa zao zilisaidia
kuwatia mbaroni wahalifu mbalimbali 30. IMETOLEWA MPEKUZI BLOG
No comments:
Post a Comment