Kikosi
cha Yanga kinatarajiwa kwenda nchini Algeria May 03 tayari kwa mchezo
wa kwanza wa kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USM Alger
utakaopigwa Jumapili May 06 huko nchini Algeria.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten
amewakaribisha mashabiki wanaotaka kusafiri na timu kwenda kuiunga mkono
nchini Algeria wajiandikishe Makao Makuu ya klabu mtaa wa Twiga na
Jangwani jijini Dar es salaam.
Baada
ya Mchezo Yanga wanatarajia kurejea nchini May 7 na kujiandaa na Mchezo
wa pili dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda utakaochezwa uwanja wa Taifa May
16.
No comments:
Post a Comment