HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday 27 April 2018

RAIS DKT JOHN MAGUFULI ASISITIZA SERIKALI HAINA MPANGO WA KUTOA CHAKULA BURE MWAKA HUU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka wananchi kufanya kazi hasa katika kilimo kwani serikali haina mpango wa kugawa chakula cha bure mwaka huu.
Rais Magufuli amesema hayo leo April 27, 2018 wakati akifungua barabara ya lami kutoka Dodoma hadi Babati, Manyara yenye urefu wa kilometa 251 ambayo imegharimu Tsh. Bilioni 378.

“Siwezi kuhangaika kutafuta fedha za kujenga barabara, kununua ndege, viwanja, alafu bado nitafute na fedha za kuwanunulia chakula cha bure. Nasema, hakuna chakula cha bure, ambaye hatalima, atakufa njaa,” amesema Rais Magufuli.

“Mvua imeenyeesha miezi yote halafu ije itokee mwezi wa ngapi mseme tunaomba chakula kuna njaa tutakufa nitasema tu kufa. Nawaambia Watanzania wote kuanzia Kongwa mpaka Chato hakuna chakula kitakachogaiwa mwaka huu,” amesisitiza.

Hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula nchini imeimarika na kufikia tani milioni 15.9 kwa msimu wa kuanzia mwaka 2016 hadi 2018 sawa na kuwa na ziada ya tani milioni 2.6 za chakula.

No comments:

Post a Comment