HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday 25 July 2014

WATU 19 WALAZWA PEMBA BAADA YA KULA SAMAKI MWENYE SUMU


Na Masanja Mabula PEMBA
Watu 19  wakaazi wa shehia ya Sizini Tumbe Wilaya ya Micheweni wamelazwa  katika hospitali ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba  wakipatiwa matibabu baada ya kula samaki aina ya pono na puju wanao daiwa kuwa na sumu.

SAMAKI BUNJU
Tukio hilo limetokea siku ya jumatano ya tarehe 23 mwezi huu  majira ya saa 12:30 za jioni katika Shehia ya  Sizini  baaa ya watu hao wa ukoo mmja kutumia samaki wakati  wa kula futari na kupelekea  hali zao kuanza kubadilika .

Baadhi ya ndugu wa jamaa waliolazwa hospitalini wamesema kuwa hali za ndugu zao zilianza kubadilika usiku majira ya saa saba na hivyo kuamua kuwakimbiza hospital kwa ajili ya kupata matibabu kunusuru hali zao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kaskazini Pemba Sheikhani Muhammedi Sheikhani amethibitisha kutokea kwa tokeo hilo na kusema kuwa waathirika wa tukio hilo wanaendelea na matibabu katika hospitalini hapo.

Aidha shekhan ametowa wito kwa jamii na kuitaka kuwa makini wakati wanapotumia samaki hasa wanaodaiwa kuwa na sumu ili kuweza kulinda maisha yao .

Kufuatia kutokea kwa tokeo hilo mbunge wa jimbo la Tumbe Rashid Ali abdallah amelezea kusikitishwa  na kuwataka wananchi wawe  na uvumilivu katika kipindi hichi na kuwataka madaktari kuongeza juhudi za kazi ili kusaidia kuokoa maisha ya watu hao .

No comments:

Post a Comment