ABIRIA
10 kati ya abiria 30 waliokuwa wakisafiri kwenye boti wakitokea Mitomoni,
wilaya ya Songea Vijinini, mkoani Ruvuma kwenda mnadani katika wilaya hiyo
wanahofiwa kufa maji baada ya boti hiyo kuzama kwenye Mto Ruvuma.
Habari zilizopatikana jana mjini
hapa zilieza kuwa, boti hiyo ilikuwa imejaza abiria pamoja na mizigo iliyokuwa
ikipekwa kwenye mnada wa hadhara ambao upo jirani na kijiji cha Mitomoni
mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Jitihada za kumtafuta Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, hazikufanikiwa baada ya kuelezwa
kuwa alikuwa ameungana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Ruvuma kwenda
kwenye eneo la tukio hilo.
Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
Mkoa wa Ruvuma, Hamis Kutiku, alisema Kamanda Mwombeji amekwenda kwenye eneo la
tukio ili kujiridhisha ukweli wa tukio hilo.
Alisema taarifa kamili juu ya tukio
hilo zitatolewa baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama kufika eneo la tukio na
kurudi mjini kwa ajili ya hatua zaidi kuchukuliwa.
No comments:
Post a Comment