Kocha wa zamani wa Azam FC Joseph Omog
raia wa Cameroon amesaini mkataba wa miaka miwili kuionoa Simba ya Dar es
Salaam, na mkataba huo utaisha mwaka 2018.
Omog
amesaini mkataba huo mchana wa leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari
akiwa pamoja na Rais wa Simba, Evans Elieza Aveva.
Omog
amesema anafahamu vyema ukubwa wa klabu ya Simba pamoja na changamoto zake na akasisitiza
atapambana kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko ingawa amesisitiza kuwa suala la
muda ni muhimu kwa kuwa kila kitu hakiwezi kubadilika siku moja.
No comments:
Post a Comment