Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Leonard
Poul, akiwaonyesha waandishi wa habari jambia na kisu silaha zilizodaiwa
kutumika katika tukio la mauaji ya watu 8 kuchinjwa na watu wanaodaiwa kuwa
majambazi tarehe 31/05 2016 kijiji cha Kibatini kata ya Mzizima Amboni Tanga.
|
JESHI La
Polisi Mkoani Tanga, limesema limekamata Silaha na vifaa mbalimbali vilivyokuwa
vikitumika kwenye matukio ya uhalifu na mauaji vikiwemo visu na majambia.
Akizungumza waandishi wa habari ofisini kwake leo, Kamanda
wa polisi Mkoani Tanga, Leonard Poul, alisema kukamatwa kwa vifaa hivyo kunatokana
na ushirikiano na vyombo vya usalama na wananchi.
Alisema kwa sasa Mapango ya Amboni yako salama kwa asilimia
mia moja na hakuna kitisho wala masalia ya majambazi na kuwataka wananchi
kufanya kazi zao za kila siku bila woga.
Amesema katika msako huo ambao ulifanywa
tangu kutokea tukio la mauaji ya watu nane huko Amboni Polisi wamekuwa
wakifanya kazi usiku na mchana na kufanikiwa kukamata watu watatu ambao walitoa
ushirikiano kwa kuonesha maficho ya silaha ambapo walikuta shehena ya silaha
zikiwemo bunduki tatu aina ya aina ya SMG, risasi 23 na majambia pamoja na
mapanga.
Pamoja na Silaha hizo Jeshi la
Polisi limekamata vyombo na madumu ya maji pamoja ,vyakula kama utumbo wa
Ng’ombe na Mbuzi ambao walikuwa wakichinja pamoja na vifaa vya kujengea zikiwemo
Sururu.
No comments:
Post a Comment