Baada ya kukubali kichapo
cha 1-0 mbele ya Mo Bejaia wiki iliyopita nchini Algeria katika(CAF)mchezo wa
kwanza wa hatua ya makundi kombe la shirikisho Afrika(CFA), Yanga sasa
wanakimbembe kingine kikubwa zaidi hapo kesho.
Mabingwa
hao wa Soka Tz Bara walimaliza msimu uliopita wakiwa na rekodi tamu ya kufungwa
mchezo mmoja 1 kati ya 30 waliyocheza na kushinda michezo 22. Kama haitoshi
Yanga walitwaa ubingwa wa kombe la FA kwa kishindo walipoichapa Azam 3-1 katika
mchezo wa fainali. Ukiangalia mwenendo huo utakubaliana nami kuwa kwa hapa
Tanzania Yanga ni kiboko yao uwanjani.
Lakini
unapozungumzia michuano ya kimataifa Yanga pamoja na vilabu vingine vya
Tanzania ni habari mbaya sana kwao kwa sababu hii ndio mara ya kwanza kwa klabu
ya Tanzania kutinga hatua ya makundi ya Kombe hili na Yanga haohao walikuwa wa
kwanza kutinga makundi klabu bingwa Afrika ambapo wakutana na vipigo vya aibu.
Michuano
ya Kimataifa kama Klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho imetawaliwa na vilabu
bora zaidi ya vilabu vya Tanzania kuanzia nje ya Uwanja mpaka ndani, nitatolea
mfano kundi hili ambalo wamepangwa Yanga, wako na Mabingwa wa Soka Afrika TP
Mazembe, Vigogo wa Soka la Algeria Mo Bejaia ambao tayari wamelamba makali yao
na Medeama ya Ghana ambayo pamoja na kuwa kwenye matatizo ya kifedha na kichapo
walichopata kwenye mchezo wa kwanzan 3-0 dhidi ya TP Mazembe bado wanaonenaka sio wakubeza mbele ya Yanga.
Tukija
kwenye mchezo wa kesho Yanga walionekana kupania sana mchezo huu kuliko michezo
mingine yote inayowakabili kwenye hatua ya makundi wanayoshiriki, lakini lazima
watambue kuwa mchezo wa soka hauongopi, mikwara na kupania sio siri ya ushindi,
zaidi inaweza kuwa aibu sana kama hawatajipanga vyema kuukabili moto wa
mazembe.
Yanga
imeweka kambi ya maandalizi nchini uturuki tangu kuanza kwa hatua hii ya
makundi, kambi ambayo imeonekana kuleta mabadiliko makubwa kwenye performance ya
timu uwanjani pale walipowakabili Mo Bejaia nchini Algeria, kama sio ubutu
kwenye safu yake ya ushambuliaji naamini Yanga wangekuwa na cha kujivunia hii
leo. Walitengeneza hafasi nyingi za kufunga hasa kipindi cha pili, nafasi
ambazo wangezipata waarabu sijui tungezungumza nini leo. Pamoja na hayo
nimewahi kushuhudia michezo kadhaa kati ya TP Mazembe na Waarabu,takribani
miaka mine sasa Mazembe wamekuwa bora kuliko Waarabu kwa kila kitu kuzuia, kumiliki
mpira na hata kushambulia, japo wameonekana kupwaya tangu waondokewe na “chinjachinja”
wa Afrika kutoka Tanzania Mbwana Samatta bado naona Mazembe ni zaidi ya Yanga.”WAJICHUNGE”
Hapa
nitatoa mbinu 4 ambazo zinaweza kupeleka furaha jangwani katika mcjezo wa kesho
ambao tayari homa yake imefikia patamu kuliko…..
1. Mbinu za Mchezo.(Game
Plan)
Mwalimu
Hans Van De Pluijm ni miongoni mwa wataalamu bora wa mbinu Barani Afrika, September
16-2012 aliiongoza Berekum Chelsea ya Ghana kuishinda TP Mazembe 1-0 katika
michuano ya CAF. Naamini anafahamu kuwa mbinu namba moja ya timu inapukuwa
nyumbani ni kutafuta kushambulia zaidi hasa kipindi cha kwanza ili
kujihakikishia ushindi huku ikikaba kwa pamoja na kuepuka michezo ya kutegea
Off Side.
Pluijm
anapaswa kuwaweka tayari vijana wake kushambulia kwa kasi na kwa umakini hasa
dakika 30 za kipindi cha kwanza angalau watangulie kwa bao 2 kisha wapate nafasi
ya kupumzika kwa dk 15 za kipindi cha pili wakizuia ili 45 za kipindi cha
kwanza zisiwaumize kiasi wakashinda kuimudu nusu ya pili ya mchezo.
Kazi
kubwa watakuwa nayo Kamusoko na Niyonzima ambao watapaswa kubance timu kwa muda
wote wakiendene na plani ya mwalimu ya kishambulia kwa dk hizo 30. Mwalimu
anapaswa kukaa nao chini na kuwaeleza kwa kina kuwa wao ndio Injini ya timu ni
kipindi gani wacheze kwenye nafasi gani.
Mbinu
ya kujilinda inaweza kuwa shubiri iwapo kutakuwa na mitego ya Off side ambayo
kuacha nafasi kubwa kati ya mabeki na golikipa na hapa wataikabili hatari ya
Washambuliaji Thomasi Ulimwengu ambaye anakasi sana akitokea pembeni na Kalaba
ambaye ni mtaalamu sana wa kulenga lango kwa mashuti ya mbali.
2. Uchezaji.(Perfomance)
Perfomance
ndo kila kitu kwenye mpira na huanzia kwenye mbinu bora za mwalimu kwa mchezo
husika. Yanga walionesha performance nzuri mbele ya Mo Bejaia lakini haikuwa na
faida kutokana na makosa ya umaliziaji.
Nikianza
na safu ya Ulinzi anaposimama Bossou na Yondani sina shaka kabisa kwa sababu
muunganiko wao umekuwa imara sana hata wanapowakabili washambuliaji hatari,
kama unakumbuka bao lililofungwa kwenye lango lao dhidi ya Bejaia lilitokana na
kukosekana kwa Boosou ambeya alikuwa nje akitibiwa kwa wkati huo.
Napata
shaka kwa mabeki wa pembeni yaani Mbuyu twite anayepewa nafasi kubwa kucheza
zaidi ya Hassan Kesy mwenye mgogoro wa kimkataba na timu yake ya zamani ya
Simba na Oscar Joshuia ambaye hayuko sawa 100% kwa mchezo huu. Mbuyu Twite
hutumia nguvu zaidi ya akili kwenye kukaba na hana faida kwa mawinga ambao
wamezoea kusaidiwa kushambulia na mwenye nafasi yake Juma Abdul ambaye ni Majeruhi.
Oscar hayuko fiti sana kucheza na hata mchezo uliopita dhidi ya Mo Bejaia
hakumaliza kutokana na maumivu ya mguu ambapo alimpisha Haji mwinyi kipindi cha
kwanza naye aliishia kupata kadi nyekundu dakika za lala salama. Wanahitaji
sana msaada iwapo itatokea wakashambiliwa mfululizo na maadui zao, mwalimu
naweza kuwashusha chini kidogo mawinga kutoa msaada.
Eneo
la kiungo wanapocheza Kamusoko, Niyonzima, Kaseke na Msuva kumekuwa na shida
sana pale timu inaposhambuliwa, ni wazuri timu ikishambulia kwa pasi zenye
macho na hata kulazimisha viungo wa timu pinzani kupoteza umakini kwenye
kuwakaba kwa kupiga pasi za haraka kwenda mbele.Mwalimu anapaswa kuwajenga upya
wajue namna ya kuficha mpira wanapoupata hasa timu inapokuwa kwenye wimbi ya
kushambuliwa na maadui, hii itasadia kupoozesha mpira na mabeki kupumzika.
Naona nafasi ya Vijana kama Mwashiuya na Mahadhi ipo pale kocha atakapoona
Msuva na Kaseke wanashindwa kuendana na kasi ya mchezo. Umri wa mdogo na kiu ya
kutaka mafanikio inaweza kuwa silaha kubwa ya kuwashinda mabeki makini wa TP
Mazembe.
Kiu
ya mashabiki wengi wa Yanga ni kumuona mshambuliaji Obrey Chirwa ambaye
anatajwa kuwa pacha wa Ngoma kutoka Plutnum ya Zimbabwe. Hii inatokana na
mfungaji bora wa klabu hiyo kwenye ligi kuu Tz Bara Amisi Tambwe kushindwa
kuonesha makali yake kwenye michuano ya kimataifa.
Ngoma
amekuwa na papara sana kwenye mechi za kimataifa hachezeshi wenzake kama
alivyokuwa akifanya kwenye ligi kuu Tz bara. Nadhamni anamipango binafsi mbali
ya ile ya timu, (aonekane na timu kubwa
aondoke yanga kwa urahisi) Mwalimu Puijm anatakiwa kufanya kazi ya ziada
kumrekebisha Ngoma kwani “Mshambuliaji mchoyo husaidia kuwalinda maadui” ikishindikana
afanye yale aliyofanya Ferguson kwa Rooney alipomshusha kucheza kiungo ili
apunguze ubinafsi.
3.Nidhamu ya
Mchezo.(Game Dicpline)
Ili
ufanikiwe kwa urahisi katika uwanja wa kivita kwenye kandanda ni vizuri umteke
mwamuzi. Njia pekee ya kumteka mwamuzi ni kutomsumbua kwa nidhamu mbovu ambayo
itamfanya awashe taa nyekundu kichwani ili asiharibu kazi yake.
Usimpe
kazi ya ziada ya kukuchagulia dhabu mara kwa mara. Wachezaji wa Yanga kama
Ngoma, Yondani na Twite wanapaswa kucheza kwa nidhamu kwa kuepuka ugomvi dhidi
ya maadui ambao wanaweza kuwatoa mchezoni na kujikuta wanafanya matendo yasiyo
ya kuingwana na hatimaye kuangukia kwenye adhabu za mwamuzi.Wakumbuke kuwa
wanamichezo mingine mbele na iwapo watapata kadi kwenye mchezo huo itaathiri
upatikanaji wa baadhi yao kwenye michezo inayofuata. Kila kadi inagharimu.
4. Uvumilivu.(Patience)
Wachezaji
wengi wa kitanzania wamekuwa na taswira kichwani kuwa wao ni wakuonewa kwenye
mkichezo ya kimataifa. Mchezaji mwenye taswira hii anaweza kupiga hata mwamuzi
jambo ambalo ni baya zaiodi kwenye mchezo wa soka. Inawezekana mwamuzi akaingia
na maamuzi mabaya dhidi yao, sasa ili waendelee kuwa salama nayeye asipate
sababu ya kuwaumiza wanapaswa kuwa wavulimivu juu ya hujuma zozote, hata zile
watakazo fanyiwa na maadui zao kama kujiangusha n.k
Nikukumbushe
mchezo wa Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil kati ya Ujerumani na Ureno, mshambuliaji
wa Ujerumani Thomas Muller alijiangusha wakati akikabiliana na beki wa Ureno Pepe kisha Pepe kwa hasira akamvamia
na kumpiga kichwa akiwa chini. Tukio hili lilimgharimu sana Pepe aliyetolewa
nje kwa kadi nyekundu.Bila ya Uvumilivu vijana wa Yanga watajikuta haiani kwa
kadi nyingio za njano hapo kesho…. “WAWE MAKINI”
Nukuu
muhimu…………
Baadhi
ya mashabiki waliosema ni wanachama wa klabu ya Simba, wamejitokeza kwenye
mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu ya Yanga na kuwataka
Wanasimba kujitokeza kwa wingi na kuiunga mkono Yanga, kesho.
Yanga inashuka dimbani kuivaa TP
Mazembe katika mechi ya Kombe la Shirikisho hatua ya Makundi kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam.Amaniel Mngonja na Rifat Maulanga wamejitokeza
kwenye mkutano huo ulioongozwa na Msemaji wa Yanga, Jerry Muro katika makao
makuu ya Yanga, Kaunda na Twiga jijini Dar es Salaam.
“Sisi sote ni mashabiki na wanachama
wa Simba, tunawaomba mashabiki na wanachama wenzetu wajitokeze kwa wingi
kuiunga mkono Yanga.“Yanga ndiyo inayoiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo,
hivyo waje kwa wingi kuishangilia,” alisema Maulanga.
Kwa upande wake, Muro alisema kwa
shabiki ambaye hataweza kuvaa jezi za Yanga, angalau avae jezi za Taifa Stars.“Kama
utashindwa basi vaa jezi ya Taifa Stars, lakini bado unaweza kuvaa jezi ya timu
yako hata kama ni Simba lakini beba bendera ya taifa, tuishangilie Yanga ni kwa
ajili ya Tanzania.”
Kuhusiana na uanachama wa Simba wa
Maulanga na Mngonja, wote walikataa kutaja kadi zao za uanachama na kusisitiza
hawakuwanazo hapo.
Takribani masaa 24
kabla ya Yanga kuwavaa TP Mazembe katika mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la
Shirikisho Afrika, meneja wa mabingwa hao wa ligi ya JK Kongo, Fredrick Kitenge
amesema hawakuja kushindana na Yanga. Kitenge ambaye huwezi kumkosa katika
pambano lolote la TP Mazembe ameiambia Soka360 kuwa licha ya kushiriki katika
mashindano ya Kombe la Shirikisho, ametamba kuwa Yanga ni wachanga mno
kushindana nao.
Ameongezea
kuwa wamekuja kutupia jicho vipaji kama walivyofanya mwaka 2011 na kufanikiwa
kumsajili Mbwana Samatta kutokea Simba na baadaye Thomas Ulimwengu aliyekuwa
Moro United kwa mkopo. TP Mazembe wamekuja na kikosi cha wachezaji 18 tu ambao
wameonekana kutukuwa na wasiwasi kabisa na pambano la kesho katika hoteli ya
Serena walipofikia.Yanga iliyoanza vibaya hatua ya makundi kwa kukubali kipigo
cha bao 1-0 kutoka kwa MO Bejaia itashuka dimbani kusaka pointi za kwanza na
kurudi katika mstari wa kupigania nafasi ya kufuzu nusu fainali.
No comments:
Post a Comment