Mji Mkuu wa
Rwanda, Kigali umetajwa kuwa Ulaya ndogo na watu tofauti kutoka barani humo na
wengine kutoka Asia kufuatia namna mji huo ulivyo.
Siku
za hivi karibuni mji huo umetangaza siku ambayo wakazi wake hawatatakiwa
kutumia magari kabisa. Kwa mujibu wa meya wa mji huo alisema kuwa siku hiyo
barabara zote zitafungwa kupisha watu kutembea wakielekea sehemu zao za kazi na
maeneo mengine.
Jumapili
iliyopita ilikuwa ni siku ya pili ya kutotumia magari ambapo watu walikua
wakielekea sehemu mbali mbali wakitembea wangine wakiendesha roller, skates,
skating boards na baiskeli.
Siku
hiyo imewekwa maalum ikiwa na lengo la utunzaji wa mazingira na kuhamasisha
watu wa mji huo kuhakikisha unakuwa safi.
No comments:
Post a Comment