Nyegere
(Mellivora Capensis) ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa duniani.
Chakula chake kikubwa ni asali,yeye hupanda juu ya mzinga wa asali na
kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na
masega yake na kula. Mwili wake una ngozi ngumu sana kiasi hata nyuki akimuuma
hakuna chochote kinatokea.
Nyegere
ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya
jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu
ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni
kuwa jani laitakuwa “limefaidi utamu” wa jike
Nyegere
anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika
wakubwa wa hasira za Nyegere,anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na
kupeleka kwa mke,mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya
kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja
mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake(ukizingatia milango ya
vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii.
Nyegere
ndio mmoja kati ya “fearless animal” duniani, huweza kuwakabili Simba na Chui
zaidi ya mmoja na kuwashinda,anasaidiwa na ngozi yake ngumu na kucha zake,
awapo katika hatari ya kushambuliwa hukakamaa na ngozi yake kuwa ngumu kama
“defensive mechanism” yake.
Kuna
makabila ambayo waganga wa kienyeji hutumia mchanganyiko wa Nyegere
kutengenezea limbwata,Yaani wamama huchukua dawa hiyo kuwawekea waume zao ili
wawe na “upendo” wa Nyegere.
Wivu
wa Nyegere hufanya awachukie sana binadamu wanaume,mwanaume ukiwa porini
ukakutana na Nyegere akiwa na jike lake jiandae kupata kibano, huona wivu kuwa
utamtamani jike,hivyo hukimbilia kumvamia mwanaume sehemu za siri akiamini
ndizo zinazokupa jeuri ya kumtamani jike lake.
Nyegere
hula nyoka wa aina yoyote,ana sumu kali ambayo akimng’ata nyoka wa aina yoyote
haponi.
Ogopa
sana kukutana na mnyama mwenye wivu Nyegere.
Huko
Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu
ya mtu aliyelina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na
kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja,akabagua yule mwizi wake, akagawa
kichapo halafu akarudi porini kimya kimya.
No comments:
Post a Comment