Waziri Wa Nchi Ofisi
ya Rais Utumishi Wa Umma na Utawala bora Mhe, Angela Kairuki amemtaka Mkuu Wa
Mkoa Wa Tanga Maritini Shegella (Pichani kushoto) kupitia tena na kuwabaini watumishi hewa ambao
bado wanaendelea kupokea mishahara huku serikali ikiwa inatumia pesa nyingi
katika kuwalipa Watu ambao hawasitahiki.
Kauli
hiyo ameitoa juzi katika kikao cha watumishi wa umma wa idara mbalimbali mkoani
hapa ambapo baada ya kupokea taarifa alipewa idadi ya watumishi hewa 198 ambao
wamebainika kupokea mishahara.
Pia
Waziri Kairuki (Pichani kushoto) amesema watumishi hao hewa wamesababisha kupoteza fedha Billion
1.5 hali iliyosababisha hasara na kukwamisha serikali kufanya kazi zake kwa
ufanisi ni vyema kupitia upya suala la kuhakiki taarifa za watumishi hewa wako
wengi mkoani hapa ni zaidi ya watumishi hewa 22,000 wamebainika hivyo amemtaka
mkuu wa mkoa wa Tanga kuhakikisha anafanya uchunguzi ili kubaini haraka kwani
ldadi hiyo imeonekana kuwa kubwa kwa Tanga.
Hata
hivyo waziri amesema katika Mkoa Wa Tanga kuna matatizo ya watumishi ambao
wanatumia vyeti feki hasa idara ya elimu na Afya wanaongoza hivyo kuzitaka
mamlaka husika kuhakikisha wanawabaini watu hao ili waweze kuchukuliwa hatu.
Aidha
amesema nijambo la kusikitisha kuona watumishi Wa serikali wanashindwa
kufanyakazi kwa weledi badala wanafanya mambo ambayo hayaendani na maadili
hivyo alisema amezuia ajira mpya zote ili kufanya uhakiki Wa watumishi kupitia
baraza la mitihani na wizara.
No comments:
Post a Comment