MABONDIA Francis Miyeyusho na Nassibu Ramadhani
wamesaini mkataba wa makubaliano wa kuzipiga siku ya sikukuu ya Pasaka katika
uwanja wa ndani wa taifa jijini Dar es salaam.
Akizungumzia mpambano uho mratibu wa mabambano hayo
Rajabu Mhamila ‘Super D’ amesema kuwa amewasainisha mabondia hao kwa kuwa
viwango vyao vipo juu sana katika kipindi hiki na ndio mpambano mkali
utakaokuwa wa kufungua mwaka 2016
Aliongeza kwa kusema mbali na mpambano huo siku
hiyo pia kutakuwa na mapambano mengine ya kukata na shoka ambapo mabondia
mbalimbali watazipiga siku hiyo.
Mohamed Matumla atavaana na Cosmas Cheka wakati
mabondia Mada Maugo atavaana na Abdalla Pazi katika mpambano wa nani zaidi kati
yao pia bondia Vicent Mbilinyi atavaana na Mwinyi Mzengela na Pius Kazaula wa
Morogoro atamenyana na Seba Temba.
No comments:
Post a Comment