Raia wa Tanzania
mwenyeji wa Mkoa wa Kilimanjaro John Baranabas ameuawa na umati mjini Nairobi baada yake
kuwashambulia na kuwaua watu wawili katika kasino.
Watu
walioshuhudia tukio hilo wanasema mwanamume huyo alikuwa amepoteza $300
akicheza kamari na kumsihi msimamizi wa kasino hiyo aruhusiwe kuweka rehani
simu yake lakini akakatazwa kwa msingi kuwa haikuwa imefikisha thamani ya
kuwekwa rehani.
Ni
hapo ambapo anadaiwa kumdunga kisu msimamizi huyo wa kasino mtaa wa Eastleigh.Mlinzi
wa msimamizi huyo alipomkabili, naye pia akamdunga kisu na kumuua.
Baadaye
alizidiwa nguvu na umati na kuuawa.Polisi wamesema mwanamume huyo mwenye umri
wa miaka 28 anatoka eneo la Rombo, mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.
Alikuwa
akifanya kazi kama fundi wa viatu kabla ya kuanza biashara ya uchukuzi wa
kutumia pikipiki, maarufu kama bodaboda nchini Kenya.Kabla ya kisa hicho,
waliokuwa wakifanya kazi naye wanasema alikuwa ameuza pikipiki hiyo.
No comments:
Post a Comment