HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Saturday, 30 January 2016

LIGI KUU YA SOKA TANZANIA BARA KUENDELEA LEO BILA AZAM.





Ligi Kuu Vodacom, VPL, Leo itapigwa tena na Mabingwa Watetezi Yanga wapo huko Mkwakwani Jijini Tanga kuivaa Coastal Union wakiwania kuzidi kupaa kileleni mwa Ligi hiyo.

Yanga wanaongoza VPL wakiwa Pointi sawa na Azam FC lakini wao wako juu kwa ubora wa Magoli na Leo ni nafasi safi kwao kuitupa mkono Azam FC ambao Mechi zao zimefutwa kwa vile wako Ziarani huko Zambia.

Leo pia zipo Mechi nyingine 5 na Jijini Dar es Salaam, Simba, ambao wako Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 6 nyuma ya Yanga na Azam FC, watacheza na African Sports ya Tanga ambayo ni ya pili toka mkiani lakini hivi sasa wamekaza buti na kuambua Sare mfululizo dhidi ya Timu ngumu Mtibwa Sugar, waliyotoka 0-0 na Azam FC, waliyopata 1-1.
Mechi nyingine hii Leo ni zile za huko Morogoro kati ya Mtibwa Sugar na Stand United, Mwadui FC v Toto Africans, Kagera Sugar v Mbeya City na JKT Ruvu kuivaa Majimaji.

LIGI KUU VODACOM
Ratiba:

Jumamosi Januari 30
Coastal Union v Yanga
Simba v African Sports
JKT Ruvu v Majimaji
Tanzania Prisons v Azam FC [IMEAHIRISHWA]
Mtibwa Sugar v Stand United
Mwadui FC v Toto Africans
Kagera Sugar v Mbeya City

Jumapili Januari 31
Mgambo JKT v Ndanda FC

Jumatano Februari 3
Kagera Sugar v Majimaji
Tanzania Prisons v Yanga
Simba v Mgambo JKT
JKT Ruvu v Mbeya City
African Sports v Mwadui FC
Mtibwa Sugar v Toto Africans
Azam FC v Stand United
Coastal Union v Ndanda FC

Jumamosi Februari 6
Kagera Sugar v Simba
Mbeya City v Tanzania Prisons
JKT Ruvu v Yanga
African Sports v Stand United

Leo Simba itaikaribisha African Sports kwenye uwanja wa Taifa, Dar  katika mchezo wa kwanza wa ngwe ya lala salama ya Ligi Kuu Tanzania Bara.Makocha wote wameweka hadharani vikosi vyao walivyopanga kuvitumia katika pambano la leo. NIPE MAONI YAKO HAPA.

KIKOSI CHA SIMBA
1.   GK.Vincent Angban
2.   Hassan Kessy
3.   Abdi Banda
4.   Hassan Isihaka
5.   Juuko Murshid
6.   Justice Majabvi
7.   Mwinyi Kazimoto
8.   Jonas Mkude
9.   Hamisi Kiiza
10.                Ibrahimu Hajibu
11.                Hajib Ugando

Akiba:
·        Manyika Peter
·        Emery Nimubona
·        Said Ndemla
·        Novalty Lufunga
·        Brian Majwega  
·        Mussa Mgosi
·        Awadh Juma

KIKOSI CHA AFRICAN SPORTS:
1.   Zakaria Mwaluko
2.   Mwaita Gereza
3.   Halfan Twenye
4.   Juma Shemvuni
5.   Rahim Juma
6.   Mussa Chambega
7.   Ally Ramadhan
8.   Pera Ramadhan
9.   Hamad Mbumba
10.                Rajabu Isihaka
11.                James Medy

Akiba
·        Faraji Kabali
·        Nzara Ndaro
·        Ally Ahmed
·        Ramadhan Msheli
·        Fadhil Kizenga
·        Hussein Amir
·        Mohamed Issa

No comments:

Post a Comment