Kilindi, MFUKO wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Tawi
la Korogwe Mkoani Tanga limetoa msaada wa mashuka 100 kwa Zahanati ya Kwediboma
Wilayani hapa kujikinga na baridi kwa wagongwa wanaolazwa kituoni hapo.
Akizungumza mara baada ya makabidhiano,
Kaimu Meneja NSSF tawi la Korogwe,
Rebule Maira, alisema msaada huo ni moja ya misaada inayotoa kwa wateja
wake vikiwemo vituo vya Afya na shule.
Alisema NSSF ilipata taarifa za kituo
kukabiliwa na uhaba wa mashuka kwa wagonjwa wanaolazwa na hivyo mfuko
kuona umuhimu wa kukisaidia na kuweza
kukabiliana na changamoto mbalimbali za wagonjwa.
Mfuko wa hifadhi ya jamii uko kwa ajili
ya jamii na leo ndio maana tumekuja hapa kusaidia jamii, tumetoa mashuka kwa
ajili ya wagonjwa kujikinga na baridi kali kama tujuavyo wilaya hii iko na
baridi kali” alisema Rebule na kuongeza
“Mfuko uko na utaratibu wa kusaidia
jamii ambapo hutenga fungu maalumu kama ujenzi wa maabara na shule pamoja na
huduma nyenginezo niwahaakikishie wananchi lengo letu nikusaidia jamii” alisema
Alisema kituo hicho kimekuwa kikipokea
wagonjwa wengi na baadhi yao kutoka Handeni na Songe pamoja na vijijini hivyo
kuyataka mashirika ya umma na Serikali kukisaidia na kuiga mfano wa Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii NSSF.
Alisema kituo kimekuwa kikipokea
wagonjwa wengi tofauti na uwezo wake na hivyo kutaka kuongeza majengo ambayo
yatakuwa na uwezo wa kupokea wagonjwa wengi wanalazwa.
“Zahanati yetu inakabiliwa na
changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa majengo ambapo kwa sasa ndio kama unavyoona
majengo tunayojenga , changamoto iko katika umaliziaji” alisema Matilda
Matilda ameitaka mifuko mengine ya Hifadhi ya Jamii na mashirika na Serikali
kukisaidia kituo hicho ili kuweza kuwapatia wananchi huduma ya matibabu na
kuondosha kero ya kufuata matibabu masafa marefu.
CHANZO:TANGA KUMEKUCHA BLOG
No comments:
Post a Comment