HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday, 12 January 2016

DIRISHA DOGO LA USAJILI 2016..TETESI ZA USAJILI HUKO BARANI ULAYA...

Arsenal wapo tayari kutoa pauni milioni 13.4 kumsajili msambuliaji wa Celta Vigo, Nolito (Mundo Deportivo),
Manchester United wameanza mazungumzo na mshambuliaji wa Atletico Madrid Saul Niguez (pichani) (Daily Mirror),
mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane amesema Spurs wana mustakbali mzuri na anataka kusalia katika klabu hiyo, licha ya kuhusishwa na kuhamia Real Madrid mwisho wa msimu (Sun),
Spurs pia watapambana na Galatasaray ya Uturuki kutaka kumsajili Loic Remy kutoka Chelsea (Daily Express),
mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino anataka kujiunga na Tottenham katika dirisha hili la usajili na atakataa dau kutoka klabu nyingine yoyote (Sun),
hata hivyo Liverpool watajaribu kumshawishi Berahino kwenda Anfield kuchukua nafasi ya Daniel Sturridge (Daily Express),
meneja wa Aston, Villa Remi Garde anataka kukibadili kikosi hicho kwa kwanza kuwaondoa nahodha Gabriel Agbonlahor na winga Charles Nzogbia (Times),
meneja wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel amesema Neven Subotic anayesakwa na Liverpool haendi popote mwezi huu (Liverpool Echo),
beki wa Leicester Ben Chilwell anasakwa na Arsenal na Liverpool (Telegraph),
mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Niklas Bendtner huenda akaondoka Wolfsburg na kwenda Newcastle United (Bild),
kiungo wa Lazio, Filipe Anderson anasema hafahamu kama atakuwepo bado Italia mwisho wa mwezi Januari (Daily Star),
licha ya kumsajili kiungo kutoka Senegal, Henri Saivet, meneja wa Newcastle, Steve McClaren anamtaka mmiliki wa klabu hiyo, Mike Ashley kuongeza wachezaji zaidi ili wasishuke daraja (Guardian),
Newcastle wametoa pauni milioni 10 kumtaka kiungo wa Swansea, Jonjo Shelvey, lakini huenda wakalazimika kulipa pauni milioni 12 kumpata (Telegraph),
Chelsea wanamfuatilia mshambuliaji wa AC Milan, Carlos Bacca, ambaye amepachika mabao manane msimu huu (Daily Mail),
Southampton wataongeza dau lao la pauni milioni 12.2 kutaka kumsajili kiungo Stefano Sturaro kutoka Juventus (Daily Mirror).





No comments:

Post a Comment