![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhLJMlhnlfuUiPSBvU7jyDfuGFiTTBxKfRHjWMpRsUbZV9Cu6fyCPJNDNc5EtijJTKDRUA1UwVkx3ZIDX8WLAGwyrS0cxJq49eJRcn58F_2QXpMv8g-0NLzKTApUsVrxhbzXhe2He7NVP8e/s320/shein.jpg)
Katika kilele cha sherehe hizo, Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein atahutubia taifa
katika uwanja wa Amaan.
Atapokea maandamano ya wananchi wa mikoa mitano ya
Unguja. Matukio mengine makubwa yatakayofanyika katika uwanja huo ni Rais Shein
kukagua gwaride la heshima la vikosi ya ulinzi na usalama, vikiongozwa na Jeshi
la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) .
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na idara ya
sherehe na mapambo iliyo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, sherehe hizo
zitahudhuriwa na viongozi wa ngazi za kitaifa akiwemo Rais wa Jamhuri ya
Muungano, John Magufuli ambaye ni mara ya kwanza kushiriki baada ya kuchaguliwa
katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana.
Ratiba hiyo inaonesha kwamba sherehe hizo,
zitahudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na
marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano na wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari, Makamu wa Pili
wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi
kusherehekea miaka 52 ya Mapinduzi, yaliyowakomboa wakulima na wafanyakazi
kutoka katika kucha za wakoloni wa kisultani.Aliwapongeza wananchi kwa
kujitokeza na kushiriki katika ufunguzi wa miradi ya maendeleo, ambayo malengo
yake ni kuharakisha maendeleo na kupambana na umasikini.
Mitaa mbalimbali mjini Zanzibar, imepambwa picha
za viongozi mashuhuri waliosimama kidete kufanya Mapinduzi hayo; hususan Rais
wa Kwanza, Abeid Amaan Karume aliyeongoza timu ya watu 16 kufanya mapinduzi
hayo.Mmoja wa walioshiriki kwenye mapinduzi, Hamid Ameir (82) , alieleza
kufurahishwa na jinsi malengo ya Mapinduzi ya mwaka 1964 yanavyotekelezwa kwa
vitendo.
No comments:
Post a Comment