Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jana, Mahiza alisema kuna kitisho cha kuzuka kwa janga la njaa na
hivyo kuwataka wakulima kujiwekea chakula ndani na pia kuwataka wafanyabiashara kuacha kuwalangua wakulima
kwa kutumia mtaji wa uhaba wa chakula.
Alisema ofisi yake inafanya
mawasiliano na ofisi ya Waziri Mkuu kuomba msaada wa chakula ili kuweza
kukabiliana na uhaba huo baada ya
mvua kuacha kunyesha hivyo
wakulima kukosa mavuno ya kutosha.
“Ndugu zangu waandishi wa habari
mbali ya kutoa salama za kuingia mwaka mpya ila nifikishieni salamu zangu
nyengine kwa wananchi kuwa kukosekana kwa mvua za kutosha kuna hatari ya mkoa
wetu kukumbwa na janga la njaa” alisema Mhiza na kuongeza
“Niwatake wananchi na wakulima kipindi hiki tusiwe na tamaa ya kujipatia
pesa kwa kuuza mazao yetu yote kwani
dalili zote za kuzuka janga la njaa liko
karibu, sababu ni uhaba wa mvua za kutosha” alisema
Pia
Mkuu huyo wa Mkoa amepiga marufuku mchezo wa Pool wakati wa kazi kwa
madai kuwa magenge hayo ni vituo vikuu vya kuuzia bangi na unga na kulitaka
jeshi la polisi na viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji kwa pamoja
kushirikiana.
Alisema mchezo huo umekuwa
ukizalisha wavutaji na wauzaji unga pamoja na kupoteza nguvu kazi za vijana
katika kujiletea maendeleo na hivyo
kusema kuwa mchezo huo uchezwe baada ya kazi nyakati za jioni.
“Napiga marufuku mchezo wa pool
kuchezwa wakati wa kazi, mchezo huu uko na vishawishi vingi vikiwemo
kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya na njama za uporaji” alisema
Mahiza
Alisema zoezi la kupiga marufuku
uchezaji wa mchezo wa poll wakati wa kazi ofisi yake inaanza operesheni mtaa
hadi mtaa na hivyo kuwataka wamiliki wa mabanda poll kujiwekea utaratibu ili
kuepuka mkono wa sheria.
No comments:
Post a Comment