YANGA
SC imevunja Mkataba na kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Hakizimana Fadhil
Niyonzima kutokana na mchezaji huyo wa Amavubi kukiuka vipengele.
Niyonzima aliwahi kuwasilisha
vielelezo vyote vya kumsafisha na kubatilisha adhabu aliyopewa Yanga SC.
Niyonzima alifungiwa kwa muda
usiojulikana Yanga SC wiki tatu zilizopita kwa tuhuma za utovu wa nidhamu baada
ya kuchelewa kurejea klabuni, kufuatia ruhusa ya kwenda kuichezea timu yake ya
taifa kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge
nchini Ethiopia mwezi uliopita.
Hata hivyo, baada ya kuchelewa
alirejea akiwa amefungwa plasta gumu (PoP) na kusema aliumia kwenye mashindano
hayo, hivyo akabaki Kigali kupata matibabu.
Lakini hiyo haikumsaidia kumuepusha na adhabu ya uongozi wa Yanga SC uliokuwa na hasira naye, ukidai imekuwa desturi yake kuchelewa kila anaporuhusiwa kwenda kwao.
Pamoja na hayo, Niyonzima
amewasilisha vielelezo vya barua pepe alizokuwa akituma kwa Katibu Mkuu wa
Yanga SC, Dk Jonas Tiboroha ambaye kwa bahati mbaya alikuwa hajibu.
TAARIFA ILIYOTOLEWA NA YANGA LEO
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiySeM8CzoQmEWjr3qxWyEeuiBUWPoxOTjCVne2VI6y3K5W1eP4Hg3TKt_dk2jE8reXmgUVFgd8wrJa5rWeQcDTtpW1BHqGIt7EsDzdlg-zNQ8nYc5wO16xlqAs7jUh3ZHpREW5IiA7fTXf/s640/1111.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhuRtt1xP1_X1BeE1uJnoYdg1d31BGcjQkiGh9iBqePfXbhadDOgYkKMOjYLL_q7ofvQiVsTHg26ibN2ZBwHObZ36CggVHEGtdt_R9vZBw8Gqdz4qdNpjSyns4Fcn9tGFq75rVl7T07n6xT/s640/yanga.jpg)
No comments:
Post a Comment