Wakizingumza katika kijiji cha Magamba baadhi
ya wakazi hao wamesema afisa wa serikali ya kijiji hawashirikisha wananchi wala
idara ya misitu wakati alipofanya zoezi hilo na badala yake ameshirikiana na
viongozi wa kamati ya ardhi ya kijiji kisha kuuza eneo hilo bila kuzingatia
sheria na taratibu zilizowekwa.
Hata hivyo mwenyekiti wa serikali kijiji cha
Magamba Bwana Salum Gumbo akielezea sakata hilo amesema yeye hakushirikishwa na
afisa mtendaji wake wa kijiji Erick Semsela kwa sababu baada ya wananchi
kuitisha kikao cha kujadili suala hilo alikimbia kijijini hapo na kwenda
kusikojulikana.
Kufuatia hatua hiyo msemaji wa familia ya
rais mstaafu Bwana Munir Juma Amoury ameziomba mamlaka husika kuchukua hatua za
makusudi kwa sababu walilipa fedha zao kwa mtendaji wa serikali ya kijiji hicho
wakiamini kuwa maeneo hayo ni salama kumbe ni hifadhi ya misitu ya asili.
SOURCE:ITV
No comments:
Post a Comment