HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 20 December 2015

SERIKALI YA MTAA WA SUMBAWANGA PONGWE YAFANYA MKUTAO NA WANANCHI NA KUIBUA HOJA NZITO



Uongozi wa Serikali ya Mtaa Mtaa wa Sumbawanga chini ya Mw/kiti wake Mr Kiswabi jana Des 19 ulifanya mkutano na wakaazi wa mtaa huo kujadili mipango ya maendeleo na changamoto mbalimbali zinazo kabili wananchi hao.
Agenda kuu za mkutano huo zilikuwa ni kero kati ya Wakulima, Wafugaji na wasio wafugaji, Usafi wa mazingira, Ulinzi na Usalama, miundo mbinu ya barabara na taarifa ya Mapato na Matumizi.
Akizungumza kwenye mkutano huo M/kiti wa Serikali ya ya Mtaa Mr Kiswabi alibainisha kuwa Halmashauri ya jiji la Tanga imetoa kipindi cha miaka mitano kwa wafugaji wote kuondoa mifugo yao ndani ya maeneo ya makazi ya watu na kwa sasa mfugaji atatozwa faini ya sh 50000/= iwapo atashindwa kudhibiti mifugo yake. Hata hivyo mmoja wa wakazi wa mtaa huo aliyetambilika kwa jina la Mama Simkoko alipendekeza iongezwe faini y ash 20000 kwa uharibifu unaosababishwa na mifugo wazo ambalo lilikubalika na mkutano huo.

Kuhusu Ulinzi na usalama kamati ya ulinzi ya mtaa huo imetoa angalizo kjwa kila mkaazi kuwa mlinzi wa mwenzake na kutoa ripoti ya matukio ya uvunjifu wa sherika kwa haraka. Kuhusu usafi wa mazingira Mkiti wa Mtaa huo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kila inapogigwa mbiu ya msaragambo wa usafi kwenye mtaa huo.
Katika hatua nyingine baadhi ya wananchi walieleza kusikitishwa kwao na hatua ya Serikali ya Mtaa huo kutoa posho y ash 10,000/= kwa wajumbe wa serikali hiyo bila ridhaa ya Wananchi.

Mmoja wa wananchi hao aliyetambulika kwa jina maarufula Bw Tiotimo ameitaka Serikali ya mtaa huo chini ya Mw/kiti wake iweke utaratibu wa kuomba ridhaa kwa wananchi kama itahitaji kutoa fedha za Serikali hiyo kwa matumizi mbalimbali, huku akihoji kwanini akidi ya wajumbe itokee upande mmoja pekee.
Akijibu hoja hizo M/kiti wa Mtaa huo amesema fedha hiyo ilitoka baada ya maridhiano ya wajumbe na taariwa ilitolewa kwenye kikao kingine huku akiwataka wananchi kujitokeza kwenye mikutano kama hiyo ili kufahamu nini kinaendelea.

Kuhusu akidi ya wajumbe kutoka upande mmoja M/kiti amesema awali kulikuwa na Mjumbe kutoka Sumbawanga B lakini hakuweza kutoa ushirikiano kila alipohitajika hivyo walimuondoa na kuweka mwingine ili kuongeza kasi ya uwajibikaji

No comments:

Post a Comment