MABINGWA wa Ulaya, FC Barcelona, Leo
wamebeba Kombe la Dunia kwa Klabu huko International Stadium Yokohama, Jijini
Yokohama, Japan baada ya kuifunga River Plate ya Argentina Bao 3-0.
Hili
ni Kombe la 5 kwa Barca kutwaa kwa 2015 baada ya kuyazoa La Liga, UEFA
CHAMPIONZ LIGI, Copa del Rey na lile la Ulaya la Super Cup na hili ni Kombe lao
3 la Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.Bao za Barca zilifungwa na
Lionel Messi, na kudumu hadi Haftaimu, na nyingine za Kipindi cha Pili za Luis
Suarez.
Katika
Mechi ya awali ya kusaka Mshindi wa 3, Wenyeji Sanfrecce Hiroshima walitoka
nyuma na kuipiga Guangzhou Evergrande Bao 2-1.Magoli ya Sanfrecce Hiroshima
yalifungwa na Douglas katika Dakika za 70 na 83 wakati lile la Guangzhou
Evergrande lilipachikwa katika Dakika ya 4 na Paulinho.
MABAO YA BARCELONA LEO YAMEFUNGWA NA LIONEL MESSI NA LUIS SUAREZ AMBAYE ALIPIGA BAO MBILI.
VIKOSI:
River
Plate: Barovero,
Mercado, Maidana, Balanta, Vangioni, Kranevittter, Ponzio, Sanchez, Viudez,
Mora, Alario
Akiba:
Chiarini, Batalla, Vega, Casco, Mammana, Mayada, MartÃnez, L Gonzalez,
Pisculichi, Bertolo, Driussi, Saviola
Barcelona:
Bravo, Alves,
Pique, Mascherano, Alba; Busquets, Iniesta, Rakitic, Neymar, Suarez, Messi
Akiba:
Ter Stegen, Masip, Douglas, Bartra, Munir, Sandro, Roberto, Adriano, Vermaelen,
Mathieu, Samper, Gumbau
REFA:
Alireza Faghani [Iran]
No comments:
Post a Comment