MABINGWA
wa Bundesliga huko Germany, Bayern Munich, wametangaza kuwa Kocha wa zamani wa
Real Madrid na Chelsea, Carlo Ancelotti, ndie atakuwa Kocha wao mpya kwa Msimu
ujao.Kocha wa sasa, Pep Guardiola, anatarajiwa kujiunga na Manchester City
ingawa hili bado kuthibitishwa na anabaki pia kuhusishwa na Man United na
Chelsea.
Hata hivyo, Kocha huyo wa
zamani wa Barcelona mwenye Miaka 44 ana nafasi kubwa kutua Etihad hasa kutokana
na urafiki wake wa karibu na Mkurugenzi wa Soka wa CitY Txiki Begiristain
pamoja na Mtendaji Mkuu Ferran Soriano, Watu ambao alikuwa nao Barcelona.
Mwezi Agosti, Man City
ilimwongezea Meneja wao wa sasa, Manuel Pellegrini, Mkataba wa Mwaka mmoja
zaidi hadi Juni 2017 lakini hilo linaonekana si tatizo kwa Guardiola kumbadili.Guardiola
alijiunga na Bayern Munich Mwaka 2013 na kutwaa Ubingwa wa Bundesliga kila
Msimu na safari hii pia yuko njiani kuutwaa kwa mara ya 3 mfululizo.
Akiwa na Barcelona, kwa
Miaka Minne, Guardiola aliweza kuiongoza kutwaa La Liga mara 3 na UEFA
CHAMPIONZ LIGI mara 1.Carlo Ancelotti, ambae amekuwa hana kibarua tangu Msimu
uliopita alipoondolewa Real Madrid, amesaini Mkataba wa Miaka Mitatu na Bayern
Munich.
No comments:
Post a Comment