HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 18 December 2015

BREAKING NEWSS>>>> BASI LAUA 12 BARABARA YA MBEYA - MOROGORO LEO..


Kuna Ajali Mbaya Sana imehusisha Basi La New Force na Lory la Mbao barabara ya Mbeya Morogoro Eneo la Ruaha Mbuyuni Wilayani Kilolo. Jumla ya watu 12 wamepoteza maisha na 28 wamejeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Peter Kakamba amethibitisha watu 12 kupoteza maisha katika ajali hiyo. Wanane ni wanaume na wanne ni wanawake. Abiria 28 wamejeruhiwa wakiwemo madereva wa basi la lori na hali zao siyo nzuri.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane alasiri ambapo basi la kampuni ya Newforce aina ya Youtong lenye namba za usajili T483CTF likitoka Tunduma kwenda Dar limegongana na lori aina ya Scania lenye namba T616DEF katika kijiji cha Mahenge, wilaya ya Kilolo Mkoa wa Iringa katika barabara kuu ya Dar - Mbeya.
Majeruhi wamelazwa hospitali ya wilaya ya Ilula, Kilomita 45 kutoka Iringa mjini.

No comments:

Post a Comment