![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgN7qzLoPRJuecsGoeYAp_2CxK1PiasViIL8Rvluipd68VpiaFX21aQYvJJx6rhx-ROcu9u2N3LT8eSEWHQ4yceMrfmrZYMvj_pLJWOd_FLev0a6SiBppgdTl9XDOq_O5Hm5tM4q0BajuZt/s640/mahiza.jpg)
Ametoa kauli hiyo
jana wakati akihoji kuhusu baadhi ya mambo aliposomewa kutoka kwenye taarifa ya
maendeleo ya wilaya ya Tanga wakati wa ziara yake ya kikazi jijini humo.
Katika taarifa hiyo
iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Abdula Lutavi alisema kwa miaka miwili
mfululizo sasa jiji hilo limefanikiwa kushika nafasi ya pili kitaifa kwa usafi
kutokana na kazi nzuri inayofanywa na wananchi kwa kushirikiana na vikundi 10
ambavyo vimeajiri vijana 110.
Mahiza alisema pamoja
na jitihada hizo bado kuna baadhi ya maeneo ya mji wa Tanga ni machafu,
yananuka na mifereji imejaa taka ngumu za mifuko ya plastiki. “Niwe mkweli tu
nitamke kwamba mitaa ya Tanga bado ni michafu, masoko machafu, mifereji imeziba
makazi ya watu ni machafu ki msingi bado sijaridhishwa na usafi kwa sababu
kipindupindu kipo hapa.
Usafi huo mmeupata
wapi acheni kulewa sifa safisheni mji “ alisema. Aidha Mkuu huyo wa Mkoa
aliutaka uongozi wa halmashauri ya jiji hilo kuitumia sheria kukataza matumizi
ya mifuko ya plastiki ambayo inaongoza katika uchafuzi wa mazingira.
No comments:
Post a Comment