Serikali kupitia wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Baraza la Taifa la Hifadhi ya Usimamizi
Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Halmashauri za Manispaa za jiji la
Dar es salaam wametangaza kusitishwa kwa muda zoezi la bomoa bomoa.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa leo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi imebainisha kuwa zoezi la bomoa bomoa limesimamishwa kwa
muda kuanzia tarehe 22,12,2015 hadi 05,01.2016.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgriGex6tpBUEmzFUow-356cSPdOhO4BunvkN8YZNmzAmnFM3staRC4IOaFm75czDxY9SiWXYPFVdg4rO1GaCeyHcYc_szzx2DltgN1NNxP8qm7tlk4MB9b6XNyrkenJiya3hhF9H8V6BEL/s320/bomoa2.jpg)
Maeneo
mengine ambayo serikali imepiga marufuku ni maeneo ya wazi, kingo za mito,
fukwe za bahari, maeneo ya hifadhi za barabara na maeneo hatarishi.
Aidha, kwa
hapa Dares salaam maeneo ya wazi takribani 180 yamevamiwa ambayo ni kama
ifuatavyo; Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni maeneo 111,
Halmashauri ya Ilala maeneo 50 na Halmashauri ya Temeke maeneo 19.
No comments:
Post a Comment