Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania
Mh.Majaliwa Kassim Majaliwa
|
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amefanya ziara ya
kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam mapema leo na kubaini upotevu wa
makontena 349.
Waziri Mkuu amebaini upotevu
wa makontena hayo ambayo yana thamani ya zaidi ya shilling bilioni 80, na
kuagiza kufutwa kazi mara moja kwa maafisa waliohusika na upotevu huo.
Majaliwa amewasimamisha kazi
Kamishna wa Kodi, Tiagi Masamaki Pamona na Habibu Mpozya wa kitengo cha huduma
kwa wateja.
Uamuzi huo wa Waziri Mkuu umekuja
baada ya kubaini kuwa katika kumbukumbu za Mamlaka ya Bandari kuna taarifa ya
makontena 349 yenye thamani ya shilingi bilioni 80 lakini taarifa hizo hazipo
kwenye kumbukumbu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Waziri Mkuu ameelekeza Polisi
kuwakamata maafisa wote waliohusika na sakata hilo kwa ajili ya hatua zaidi za
kisheria.
No comments:
Post a Comment