HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Friday, 27 November 2015

SHERIA YA ELIMU YATAKIWA KUFANYIWA MAREKEBISHO VISIWANI ZANZIBAR.



Na Masanja Mabula.ZANZIBAR
AFISA Ustawi wa Jamii Wilaya ya Wete Haroub Seleiman amesema iko haja kwa sheria ya elimu kufanyiwa marekebisho ili iweze kutoa adhabu kali kwa wazazi wanaowakatisha masomo watoto wao kwa ajili ya kuolewa .

Amesema kuwa sheria hiyo bado ina mapungufu jambo ambalo linasababisha wazazi na walezi kuwakatisha masomo  watoto wao ili waolewe

Akizungumza na mtandao huu  kuelekea kwenye maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto , Haroub amesema kuwa mtoto akiwa shule huwa chini ya usimamizi wa wizara ya elimu .

Aidha amesema kwamba katika kufanikisha udhibiti wa ndoa za umri mdogo , Haroub ameishauri jamii kushirikiana na taasisi husika kwa lengo la kulinda maslahi ya watoto .

Naye Mwenyekiti wa kamati ya hifadhi ya mtoto Wilaya hiyo bi Sada Suleiman ameitaka jamii kuacha tamaa ya utajiri kwa kuwakatisha masomo watoto wao na kisha kuwaozesha .

No comments:

Post a Comment