Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr John Magufuli amemteua Mbunge wa Ruangwa Majaliwa
Kassim Majaliwa (Pichani) kuwa Waziri Mkuu wa awamu ya tano ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Uteuzi
wa Mh Majaliwa Kassim kuwa Waziri Mkuu umekuwa tofauti kabisa na ilivyokuwa
inadhaniwa na wananchi wengi kwani jina lake halikuwa miongoni mwa majina
yaliyokuwa yakitajwa sana.
Akisoma
barua iliyokuwa na jina iliyowasiliswa bungeni mapema leo na mpambe wa Rais,
Spika wa Bunge Mh Job Ndugai alisema kuwa barua hiyo ilikuwa ndani ya bahasha
tatu tofauti.
Aidha,
Rais Magufuli aliandika kwa mkono wake mwenyewe, barua hiyo haikuchapwa kama
ilivyozoeleka.
Majaliwa
Kasim ambaye alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwenye Serikali
ya awamu iliyopita, jina lake litathibishwa na bunge leo Alhamis Novemba 19 kwa
kupigiwa kura za ndio au hapana.
Majaliwa
Kassim ana umri wa miaka 54, amezaliwa Disemba 22, 1960, amekuwa mbunge wa
Ruangwa tangu mwaka 2010.
Baada
ya kuthibitishwa na Bunge, Kassim Majaliwa ataapishwa na Rais John Magufuli
kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya awamu ya tano.
Aidha
kwa upande wa ratiba ya bunge, baada ya zoezi la kumthibitisha Waziri Mkuu
kukamilika, wataendelea na zoezi la kumchagua Naibu Spika ambapo Dr Tulia
Ackson aliyepitishwa na CCM kuwania wadhifa huo, anatarajiwa kuibuka kidedea
kutokana na idadi kubwa ya wabunge wa chama hicho bungeni.
Hali ya Bunge baada ya kutajwa kwa jina la
Kassim Majaliwa lililipuka kwa shangwe kwa wabunge wote kwani hawakutegemea na
kuwa hali ya ‘surprise’.
No comments:
Post a Comment