NA REBECA DUWE.
Kilindi TANGA.
WATOTO
wanne Jamii ya Kimasai wa Kijiji cha Lukole Kata ya NegeroTarafa ya Kimbe wilayani Kilindi Mkoani Tanga wamefariki dunia huku
mwenzao mmoja akinusufika wakati wakiogelea kwenye bwawa kubwa
lililochimbwa na Wafugaji wa eneo hilo kwa ajili ya kuhifadhi maji ya kutumia katika shughuli za ufugaji.
Akizungumza,Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Zuberi Mwombeji(Pichani)
alisema kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 16 mwaka huu nyakati za
asubuhi katika kijiji hicho wakati vijana hao ambao walikuwa watano
walipokwenda kuchunga mifugo yao.
Alisema kuwa ulipofika muda wa mchana vijana hao walifika katika eneo hilo lililokuwepo na bwawa ,ambapo vijana hao walikwenda kwa lengo la kunywesha mifugo yao na baada ya tukio hilo waliamua kuvua nguo na kuogelea wakati mwenzao waliyekuwa naye akiwasubiri na ndipo walipozidiwa na maji na kuzama na kutokuonekana tena.
Kamanda Mwombeji aliwataka vijana hao kuwa ni Kizito Kaduti miaka (8),
Samweli Salulu (12), Godwin Labole (12) ambaye ni mwanafunzi wa Darasa
la pili shule ya Msingi Lukole na Ole Cheusi (6) ambao walikufa wakati
walipokuwa wakiogelea kwenye bwawa hilo.
Aidha Kamanda huyo alisema baada ya kutokea kwa tukio hilo ndipo mwenzao ambaye walikuwa wameambatana naye kwenye uchungaji huo aliyejulikana kwa jina la Pendaeli Cheusi (5) alirudi nyumbani na
kuwajulisha wazazi wao.
Aliongeza kuwa baada ya wazazi kupata taarifa hizo waliweza kwenda
kwenye eneo la bwawa hilo na kukuta miili ya watoto wao ikielea juu
ya bwawa hilo ambapo kwa sasa uchunguzi wa madaktari unaendelea na
taratibu nyengine
Aidha kamanda Mwombeji aliwataka wazazi na walezi kuwa makini na watoto wao hususani katika kipindi hiki cha mvua zinazo endelea kunyesha ili kuweza kuepukana na vifo visivyo vya lazima
Wakati huo huo Jeshi la Polisi Mkoani hapa linawashikilia
wafanyabiashara watatu waliokamatwa na madawa ya kulevya aina ya Mirungi kg 530 wakiisafirisha kutoka Mombasa nchini Kenya kuyaingiza
Mkoani Tanga kwa ajili ya matumizi.
Kamanda Mwombeji alisema kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 16 mwaka
huu saa kumi na nusu jioni eneo la Mpirani Kata ya Chongoleani Tarafa
ya Chumbageni jijini Tanga katika barabara ya Tanga-Mombasa wakati
polisi wakiwa kwenye doria zao.
Alisema kuwa Polisi wakiwa kwenye doria hizo ndipo walipoliona basi
hilo na kulisimamisha na kuanza kulipekua na kufanikiwa kukuta mirungi
hiyo iliyokuwa imefichwa kwa kuchanganywa na majani ya migomba ya
ndizi kitendo ambacho kilikuwa sio rahisi kuonekana.
Aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Mohamed Omari (26) mkazi wa barabara
14 jijini Tanga,Haruna Hamisi (31) mkazi wa Tamta Jijini Tanga na
Azizi Athumani (27) mkazi wa Jijini Dar es Salaam ambao walikuwa
wakisafirisha mirungi hiyo kwenye basi lenye namba za usajili T.567
CMU aina ya Scania mali ya Kampuni ya Smart iliyokuwa ikitokea Mombasa
Kenya kuja Jijini Tanga.
Alisema kuwa watuhumiwa hao wote wamekamatwa na wanashiliwa kwenye tukio cha Polisi Chumbageni kwa ajili ya taratibu zinazofuata ikiwemo kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakibili.
No comments:
Post a Comment