Wakazi wa Magaoni kata ya Mabawa Tanga wakiangalia nyumba zao
zilizozingizwa na maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku wa leo na kusababisha kuyahama
majumba yao.
Mvua hiyo inayodaiwa
kunyesha kuanzia saa 9 usiku inasemekana kuwa kubwa kuwahi kunyesha kwa siku za
hivi karibuni.
Baadhi ya wanaharakati na
kada mbalimbali wamewataka wananchi wanaoishi mabondeni na kando kando ya
mabwawa kuchukua tahadhari na kuchimba mifereji ili kuyawezesha maji kupita kwa
urahisi bila kuathiri majumba yao.
Kwa upande wa Serikali
imekuwa ikitoa tahadhari kwa watu kuacha kujijengea nyumba bila kufuata
taratibu za mipangomiji jambo ambalo limekuwa likipelekea kujenga kienyeji na
nyakati za mvua maji kuingia majumbani mwao.
CHANZO> TANGA KUMEKUCHA BLOG.
No comments:
Post a Comment