Tanga,POLISI Mkoani Tanga, imewakamata wahamiaji haramu 45 wenye
asili ya Kiethopia wakiwa katika gari aina ya fuso baada ya kuwepo kwa taarifa ya watu hao kusafirishwa kutoka Moshi Mkoani
Kilimanjaro kueleka Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana,
Kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji, alisema tukio hilo lilitokea
juzi saa 6 usiku katika kizuizi cha polisi cha Mombo Wilayani Korogwe.
Alisema watuhumiwa hao waligundulika wakiwa wamefichwa
katika gari aina ya fuso ambalo mlangoni na pembezoni mwa gari iliwekwa mikungu ya ndizi ili kuwaficha lakini polisi
ilitilia shaka baada ya kusikia minong’ono ya sauti za watu ikitokea ndani ya
gari.
Kamanda Mombeji aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni, Mlacho
Mathias (24) Oleso Bafe (22) Dameke Lodore (20) Damekglo Achore (20), Jose
Yosete (25), Tarafa Kajamo (18), Aserat Eleysa (17), Dagu Sumoro (40), Akililu
Abeba (22), Aberhame Tadewose (20),
Abara Adese (30) , Ayrno Bekele (20),
Taseme Workicho (20), Adam Ashore (21), Tamasegen Tumoro (19), Baharu
Detamo (21), Sekadu Ababea (23), Wondem Wakere (24), Tamerat Dafar (21), Beruke
Kelebore (21), Nuruden Tamso (22), Dekebe Abebe (17), Mulegeta Alam (20),
Chakebo Muhaba (22), Alamayu Tasama (23), Manegestu Marko (24), Kayadayn Nourgaba (24), Eleyas Eregano
(24), Tasama Herama (18), Adese Kate (22), Daraje Damaka (22), Ramato Atoro
(23), Damake Damerati (25), Workicho Kidir (20), Tamasgen Lamango (20),
Sambatno Asafa (23), Takatare Tsagaye
(22), Takala Aniko (17), Kabada Tadewose (16), Mide Mhamade (25) Dandem
Deledele (23), Dagenet Wolede (25) , Gelachu
Tadese (20), Lere Abdella (18) na
Thomas Kibamo (21).
Alisema watuhumiwa wote wanashikiliwa kituo kikuu cha Polsi
cha Chumbageni na wanahojiwa na mara baada kukamilika upelelezi watafikishwa
mahakamani kujibu tuhumza za kuingia nchini bila kibali.
Alisema mbali ya wahamiaji hao pia inawashikilia Watanzania
watano kwa tuhuma za kuwasafirisha Waethopia hao akiwemo dereva wa Fuso Khamis
Ally (31) mkazi wa Kinondoni Dar es Salaam pamoja na utingo na watu waliokuwa
ndani ya gari hilo.
Aliwataja watu hao kuwa ni Ally Haruni (17) ambaye ni utingo
mkazi wa Tegeta, Mussa Shaban (30) fundi gari mkazi wa Kinondoni MkwajuniYohana
Teherera (22) mfanyabiashara wa Dar es Salaam na Fadhilui Hussein (27) fundi muashi na mkazi wa Muheza Tanga.
“Wale wahamiaji walikuwa wamewekwa katika fuso huku mlangoni
walikuwa wameweka mikungu ya ndizi pamoja na pembezoni kwa ubavu wa gari ili
kuwalaghai polisi njiani ambapo njama zao ziligonga mwamba” alisema Mombeji na
kuongeza
“Wakati gari iliposimamishwa na askari wanalikagua
walipoulizwa wakadai kuwa wamepakiza ndizi na kupeleka Dar es Salaam---mara
wakasikia watu wanakohowa na minong’onomong’ono na kugundua rundo la watu
ndani” alisema..
Kamanda alisema watu wote wanashikiliwa na polisi kituo
kikuu cha Chumbageni pamoja na gari kwa mahojiano na mara baada ya upelelezi
kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhumza za kusafirisha wahamiaji
haramu.
Imetoka:TANGA KUMEKUCHA BLOG
No comments:
Post a Comment