Tume ya Taifa ya Uchaguzi imewaasa wapiga kura
kote nchini kuhakiki taarifa zao katika vituo vya vya kupiga kura siku nane
kabla ya uchaguzi.
Hayo yamesema jana Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva (pichani kushoto) alipokuwa akizungumza katika
mkutano na viongozi wa vyama vya siasa uliyofanyika Oktoba 12, 2015
jijini Dar es Salaam.Jaji Lubuva amesema kuwa lengo la mkutano huo ni
kushauriana na vyama vya siasa katika kuelekea siku ya uchaguzi mkuu
utakaofanyika oktoba 25 mwaka huu.
“Tume imepanga kuhakikisha
kila mpiga kura mwenye sifa ya kupiga kura anapata haki ya kupiga
kura na imeagiza wasimamizi wa kura kutoa nafasi za upendeleo kwa watu
wenye ulemavu wa aina mbalimbalina na imeandaa karatasi maalum za kupigia
kura kwa watu wenye walemavu wa kuona”,alisema Jaji Lubuva.
Aidha Jaji Lubuva
aliwasihii viongozi hao kunadi sera zao majukwaani badala ya kuilalamikia Tume
katika majukwaa wakati wa kampeni pia amewasaa wanasiasa hao
kupeleka malalamiko yao katika ofisi husika na kuacha kukimbilia
waandishi wa habari.
Mbali na hayo Mwenyekiti wa
Tume hiyo aliendelea kusisitiza juu ya viongozi wa vyama vya siasa wanao
walazimisha wapigia kura kubaki katika vituo vya kupigia kura kuacha kauli hizo
kwani kwa uzoefu unaonyesha kwamba wafuasi wa vyama wanapokutana pamoja huweza
kuchangia uvunjifu wa amani.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa
Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw.Kailima Ramadhani alisema Tume ilibani
kuwa jumla ya watu 3,870 walioandikishwa hawakuwa raia wa Tanzania na hivyo
vitambulisho vyao vimerejeshwa Tume na taarifa zao kufutwa kwenye kanzidata ya
daftari la kudumu la kupiga kura.
“Katika kuelekea uchaguzi
Tume imeandaa vituo vya kupigia kura 65,105 ambapo Tanzania Bara ni vituo
63,525 na Zanzibar ni vituo 1,580 kila kituo kitakuwa na uwezo wa
kuhudumia wapiga kura 450 na kituo kitakacho kuwa na wapiga kura zaidi ya 500
kitagawanywa katika vituo viwili,”alisema Bw.Ramadhan.
Mpaka sasa tume
imeshasambaza vifaa mbalimbali vya uchaguzi nchini, vifaa ambavyo
havijasambazwa ni pamoja na karatasi za kura, wino maalumu, karatasi za matokeo
na muhuri wa kituo kutokana na umuhimu wake ila vinatarajiwa kuisambazwa hivi
karibuni.
No comments:
Post a Comment