Jana Cristiano Ronaldo (Pichani) alitunukiwa Buti ya
Dhahabu ya kwa Ufungaji Bora huko Ulaya na kuweka Rekodi kwa kuitwaa mara 4.
Msimu
uliopita, wa 2014/15, Ronaldo alifunga Bao 48 kwenye La Liga na kutwaa Buti ya
Dhahabu kwa mara ya 3 akiwa na Real Madrid wakati mara moja alitwaa Msimu wa
2007/08 akiwa na Manchester United.
Hii ni
mara ya kwanza katika Historia ya Miaka 47 ya Tuzo hii ya Buti ya Dhahabu kwa
Mfungaji Bora wa Ligi za Ulaya kuichukua mara 4.Mpinzani wa jadi wa Ronaldo,
Lionel Messi, ameshika Nafasi ya Pili kwa kufunga Bao 43 katika La Liga Msimu
uliopita.
Wakati
akikabidhiwa Tuzo yake hiyo, Ronaldo alisindikizwa na Mama yake, Mtoto wake,
Kocha wa Real Madrid, Rafa Benitez, Rais wa Real Florentino Perez na Balozi wa
Portugal huko Spain.
Hivi
sasa Ronaldo, mwenye Miaka 30, ameifungia Real Jumla ya Mabao 323, sawa na
mshika Rekodi wa Bao nyingi katika Historia ya Real, Raul, lakini Jumamosi Staa
huyo ana nafasi ya kumpiku Raul wakati Levante ikienda Santiago Bernabeu kuivaa
Real kwenye La Liga.
No comments:
Post a Comment