Na Rebeca Duwe, Tanga.
WAJASIRIAMALI
wanawake wanaofanya biashara ndogondogo za kuvuka mipaka ya
nchi wametakiwa kujiunga na majukwaa yayonawezesha kupata elimu itakayowezesha
kuwatetea wakati wa kwenda ng’ambo kupitisha bidhaa zao za biashara bila
kunyanyaswa kwa namna moja ama nyingine.
Mkurugenzi
mtendaji wa TWCC akizungumza na wanawake
waliohudhuria
katika semina la jukwaa la Horororo
wilayani mkinga mkoani Tanga hivi karibuni.
|
Hayo aliyasema mkurugenzi mtendaji wa Tanzania women Chember
Of Commerce (TWCC) Bi Flora Rimoy katika Semina ya Jukwaa la Horohoro ya
elimu ya jinsia iliyotolewa kwa wanawake mkoani hapa , ilifanyika katika
wilaya ya Mkinga katika Ukumbi wa World vision kwa muda wa siku mbili hivi
karibuni.Semina hiyo ambayo imefundishwa na Mwl. Magreth Mahenge aliyeambatana
na mkurugenzi huyo kutoka kampuni inayojihusisha na kuendeleza biashara
ya wanawake wajasiriamali wa Tanzania ambapo walihudhuria wanawake
takribani 32 kutoka wilaya tatu za mkoa wa Tanga ikiwemo Wilaya ya Muheza ,
Mkinga na Tanga.
Aidha Mwl.Mahenge aliwahimiza wanawake kutafuta elimu juu
ya haki zao ili kuondokana na unyanyasaji wakati wa usafirishaji wa
bidhaa zao bila kuogopa wala kujidharau kwani bila kujua sheria na
taratibu za kuvuka mipaka ya nchi wanawake ni vigumu kufanya biashara kwa uhuru
hasa katika utozwaji wa ushuru isiyostahili kulingana na mzigo
unaosafirishwa na umda uanaotakiwa kufika kwa mjasiriamali anayehusika.
Tanzania Women Chember of Commerce (TWCC)NI Kampuni
inayojihusisha na kuendeleza biashara za wanawake wajasiriamali wa Tanzania ,
ambayo haimiliki hisa za fedha wala kutengenza faida kutokana fedha inyotolewa
huzungushwa kuendesha kampuni na haitolewi kama gawio kwa Mujibu wa maelezo
kutoka Mkurugenzi mtedaji bi. Rimoy.
Hata hivyo alisema kwa tafiti iliyofanywa TWCC imebaini kuwa
Changamoto nyingi ambalo inawakabili wanawake wengi ni kushindwa
kutambulika na kutopata huduma za kutosha na sahihi toka vyombo mablimbali kama
Mabenki Serikali na wadau wengine wa maendeleo .
Aidha alisema kukosekana au kutokana na uwakilishi dhaifu wa
masuala ya wanawake ndipo ilipozaliwa TWCC,ambapo inaendeshwa au
kusimamiwa na bodi ya wakurugenzi na kazi za kila siku inayofanywa na
mkurugenzi mtendaji.Sanjari na hayo alisema kuwa uanachama uko wazi
kwa mwanamke yeyote mfanya biashara halali kupitia kampuni yake
binafsi au kuwa mwanachama wa chama cha biashara klilichosajiliwa, hivyo
ni lazima kutimiza vigezo vya kimsingi kama ilivyoainishwa na bodi na
kuhakikiwa na mkutano mkuu wa TWCC.
Wanawake waliohudhuria wakifuatilia kwa makini masomo katika semina ya jukwaa la horohoro wilayani mkinga mkoani hapa. |
Aidha alieleza kuwa Dhamira ya TWCC ni kuwa kitovu cha
kichocheo katika kumkomboa mwanamke mfanya biashara wa kitanzania
kiuchumi ambayo pia ina dhamira ya kuandaa wanawake wa Tanzania kuwa na
umoja wa kutetea haki na kukuza biashara zao kwa kutumia fursa na mikakati
ndani ya nje ya nchi.Alisema TWCC ina malengo ya kuwawezesha wanawake kupambana
kikamilifu ili kukuza uchumi na kuwaondolea umaskini , kuwawezesha wanawake
kuona fursa mablimbali za kibiashara na kuzitumia ili kuwa na biashara
endelevu pamoja na kuwaelekeza wanawakae jinsi ya kupata taarifa za kukuza soko
la biashara ya ndani na je.
“kusaidia ukuaji wa wanawake wajasiriamali endelevu na
kulinda haki na maslahi ya wajasiriamali hao ni kuchangia maendeleo ya
ukuaji wa uchumi wa wa Tanzania” alisema Rimoy.
Jukwaa la horohoro ilizinduliwa rasmi
tarehe 4 mwezi November 2014 ambapo inaendelea kuwahamasisha
wanawake kujiunga na jukwaa hilo ili washirikiane kutatua changamoto zinazo
wakabili wanawake hususani elimu ya Jinsia na namana ya kukuza uchumi wao.
Katika harakati za kumkomboa mwanamke hasa katika sekta ya
soko la ajira nchini Tanzania UN,ilianzisha mikakati ya kufadhili mradi
ulioanzishwa mwaka 2012 hususani kutatua tatizo la ajira kwa vijana wa
kike ili kujikwamua kimaisha na kuepuka utegemezi.Alisema kuwa mipaka amabao
hutumika kuvusha bidhaa zao ni kumi na moja (11) amabapo kila mpaka una
jukwaa lake, ikiwemo mpaka wa Horohoro,Holili,Namanga, Sirari , Mutukula
, Mwanza, Rusumo,Kibanga Kigoma , Mtwara na Tunduma.
Wanasemina wakiwa katika picha ya pamoja wawezeshaji wa semina hiyo mara baada ya semina iliyofanyika wilayani Mkinga Mkoani Tanga. |
Hata hivyo baadhi ya wanawake waliohudhuria katika Semina
hiyo akiwemo Hadija Fusi kutoka Wilayani Muheza na Selina Ndomba kutoka Tanga
kwa pamoja waliipongeza jitahada hizo ambazo zimefanywa na TWCC ya kutoa
elimu ya jinsia kwa wanawake hao hususani kuwahamisisha wanawake kujiunga
na Jukwaa la Horohoro ili wapte elimu ya kupata haki zao , hasusan haki
ya kumiliki mali katika familia kwani mwanamke ndio mwalimu wa familia.
No comments:
Post a Comment