Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa imewaasa na
kuwataka viongozi wote wa vyama vya siasa kutoa kauli na maelekezo
kwa wafuasi wao na wanachama wa vyama vyao kutoshiriki katika aina yoyote ile
ya uvunjifu wa amani hususan katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu na
baada ya uchaguzi huo.
Hayo yamesemwa leo na Msajili
wa Vyama Vya Siasa, Jaji Francis Mutungi wakati akizungumza na waandishi wa
habari leo kwenye ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi hiyo jijini Dares
Salaam.
“Dhamana ya nchi iko mikononi
mwenu,ushawishi wenu kuhusu amani katika kipindi hiki ndio utakaoliokoa taifa
la Tanzania ama utaliingiza taifa katika vurugu na mfarakano,” alisema
Jaji Mutungi.
Jaji Mutungi alisema katika kipindi
cha kampeni kumekuwepo na viashiria vya uvunjifu wa amani miongoni mwa jamii
yakiwemo baadhi ya makundi ya wanachama, wafuasi na mashabiki wa vyama siasa.
“Makundi hayo yanadiriki kutoa
maneno ya kejeli, matusi, kuvamia, kupigana, hata kujeruhi makundi mengine,
ambayo siyo ya upande wao. Hali iiachwe mara moja ili kuiweka nchi yetu
Tanzania katika hali ya amani na kuiepusha kuingia kwenye vurugu,
mfarakano na machafuko yasiyokuwa na ulazima.
“Dumisheni amani na kamwe
tusijiingize kwenye siasa zinazoleta mfarakano na uvunjifu wa amani,
kumbukeni kuna maisha baada ya uchaguzi na amani ya nchi yetu ni
fahari yetu sote,alisema Mutungi.
Aliongeza ni vyema Watanzania,
wakatambua kwamba utofauti wa itikadiya vyama ndio ukomavu wa demokrasia nchini
hivyo ni jambo la busara kuvumiliana na kufanya siasa za
kiustaarabu.Hivyo kutovumiliana kwa utofauti wetu wa itikadi za kisiasa
kunaweza kulata madhara makubwa kwa jamii itakatopelekea idadi kubwa ya
Watanzania kupata athari ikiwemo ulemavu, vifo, ukimbizi,njaa na maradhi.
Aidha ofisi hiyo imetoa rai kwa
waandishi wa habari watumie kalamu zao vysema kuhubiri amani na kuepuka
kuandika habari za uchochezi, bali wawasaidie wananchi kupata taarifa sahihi
zitakazowasaidia kufanya maamuzi wakati wa kuchagua viongozi wao.Kwa upande wao mabalozi wa amani,
ambao ni Mrisho Mpoto na Christina Shusho walisema kwa nyakati tofauti kuwa
wamejitolea kuhubiri amani kupitia fani yao ili nchi yetu iendelee kuwa
na amani.
Akizungumzia suala hilo, Mpoto
aliwapa changamoto waandishi wa habari wajiulize kuwa wana mchango
gani katika nchi yao ili kuhakikisha inakuwa na amani. Hivyo wanapoandika
habari yoyote wakumbuke kwamba kuna watoto, yatima, walemavu na wajane,
isije ikawa ni chanzo cha kuvuruga amani.
Naye Shusho alisema kwamba yeye si
mfuasi wa chama chochote,bali balozi wa kuhubiri amani.
Ofisi hiyo imetoa kauli hiyo, kwa
kuwa ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha ukuaji wa demokrasia unakuwepo kulingana
na sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kikatiba.
No comments:
Post a Comment