Na Mariam Cyprian,Tanga
SERIKALI imekitaka chuo cha utumishi wa umma kuhakikisha
mafunzo na shauri za kitaaluma zinazotolewa zinalenga katika kukabiliana
na changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya kitanzania.
Rai hiyo ilitolewa na Naibu katibu mkuu,Ofisi ya
raisi,menejimenti ya utumishi wa Umma Hab Mkwizu (pichani kushoto)wakati wa mahafali ya 23 ya
chuo cha utumishi wa umma yaliyojumuisha matawi yote nchini na kufanyika jana
jijini hapa.
Mkwizu alisema maboresho katika sekta ya umma
yatawezesha watumishi waliopo serikalini na watumishi watarajiwa kukabiliana na
utandawazi unaoendelea duniani.
“Mmekuwa nguzo ya msingi katika kuandaa utumishi wa
umma uliotukuka ambayo ni nguzo ya maendeleo endelevu lakini pia chuo
kimefanya tafit mbalimbali zilizoiwezesha serikali kuandaa sera nzuri za
mafunzo ambayo yanaendana na kasi ya mahitaji yatokanayo na
utandawazi”alisema Mkwizu
Naye Mtendaji mkuu wa chuo cha utumishi wa umma
Tanzani Said H.Nassoro alisema uongozi wa chuo hauna budi kufuata maelekezo
yaliyotolewa na raisi wa jamhuri ya muunga wa Tanzani Jakaya Kikwete
wakati wa maadhimisho ya miaka kumi ya tume ya utumishi wa umma.
“Jukumu la chuo cha utumishi wa umma ni kutoa
mafunzo kwa watumishi wote wa umma kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu… lakini
pia tangu chuo kilipo anzishwa kimeendela kufanya kwenye maeneo mbalimbali ikwa
ni pamoja na upanuzi wa chuo pia tunatarajia kufungua tawi jipya kanda ya
ziwa”Alisema Nassoro
Kwa upande wake Mkurugenzi wa tawi la Tanga Hassan
Issaya alisema kuwa wanauomba uongozi wa wizara pamoja na serikali kwa ujumla
kusaidia kuendeleza tawi la Tanga kwa kuwa imeonekana mkoa huo kuwa mzuri kwa
shughuli za chuo kutokana na mwitikio wa wanafunzi.
No comments:
Post a Comment