Na
Mariam Cyprian,Tanga
Serikali wilayani Bumbuli mkoani Tanga imetakiwa kushirikiana na secta
binafsi katika kuhakikisha wanaleta maendeleo kwa wananchi wa wilaya
hiyo pamoja na halmashauri hiyo.
Hayo yamebainishwa na afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya wilaya
ya Bumbuli Dameck Butoto wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa ofisi
ya wasaidizi wa kisheria iliyozinduliwa wilayani humo na shirika
lisilo kuwa la kiserikali la EQUALITY FOR GROWITH kwa lengo la
kuhamasisha na na kulinda haki za wafanyabiashara masokoni hususani
wanawake.
Butoto alisema serikali pekee haiwezi kutekeleza kila jambo kutokana
na ufinyu wa rasilimari fedha na watu hivyo ni vema ikasaidiana na
secta binafsi ambazo ni wabia wa maendeleo katika kuhakikisha wananchi
wanapata huduma mbali mbali za kijamii.
''Natambua msaada wa kishera uliokwishatolewa kwa viwango vya taaluma
ya sheria ndio maana nasisitiza jitihada ziongezwe ili kufikia lengo
lililokusudiwa na mradi huo” alisema Butoto.
Kwa upande wake Afsa mradi kutoka shirika EQUALITY FOR GROWITH GastonMtitu ,alisema kwamba tangu mradi huo ulipo anzishwa katika halmshauri
hiyo mwezi NOVEMBA 2014 umefanikiwa kutoa huduma ya msaaada wa
kisheria kwa wajasiliamali 114 na kutoa elimu ya kisheria kwa
wajasilia mali 323 wengi wao wakiwa ni wanawake.
Aidha afsa mradi huyo alisema kwamba mradi huo utaendeshwa kwa muda wa
miaka mitatu na shirika linawajibika kutoa mafuzo ya siku 25 kwa
wasaidizi wa kisheria 25 ambao watakuwa chachu ya kusambaza huduma za
kisheria hasa kwenye vikundi vya kiuchumi kama vile vikoba
Nao baadhi ya washiriki wa mafuzo hayo ambao pia ni wakazi wa wilaya
hiyo ya bumbuli walisema kuwa kutokana na mafunzo walioyapata
wameshatatua zaidi ya migogoro mia moja ikiwemo migogoro ya ndoa,
aridhi, mirathi na matunzi kwa watoto.

No comments:
Post a Comment