Na Mariam Cyprian,Tanga
MUUNGANO wa Chama cha Wasafirishaji Abiria Jijini Tanga(MUWATA) kimewataka
wamiliki wa magari, Madereva na makondakta kuacha kujiingiza na kushabikia
masuala ya siasa kwa kupitiliza katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi kwani
kufanya hivyo watashindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa wananchi.
Akizungumza jana,Mwenyekiti wa chama hicho,Hatwabi Shabani
alisema kuwa wameamua kutoa kauli hiyo kwa jamii hiyo ili kuweza kutoa huduma
zao ipasavyo kwa wananchi wa Jiji la Tanga bila kujali itikadi zao ili
kuhakikisha huduma wanazozitoa zinakuwa na tija kwa wahusika wote.
Alisema kuwa lazima watambua kuwa wao kama watoa huduma
wanapaswa kutokuwa na mrengo wa vyama vya aina yoyote vya siasa na badala
yake wawe mfano wa kuigwa kwa abiria ili kuhakikisha wanaleta amani katika
vyombo vyao vya usafiri.
“Tunajua kuwa muamko wa siasa kwa sasa umeongezeka hivyo
ombi letu kwenu ni kuhakikisha kwenye magari yetu tunakuwa mfano wa kuendeleza
amani iliyopo inaendelea kudumishwa na sisi kama watendaji wa magari tujiepushe
na ushabiki wa kupitiliza kwani unaweza kusababisha migogoro “Alisema Hatwabi.
Alisema kuwa jamii hiyo ina wajibu mkubwa kuwahudumia
wananchi jambo ambalo linaweza kutoa taswira mbaya na kusababisha vurugu
zisizokuwa za lazima ndani ya magari wakati wa utoaji wa huduma zao.
Hata hivyo alisema kuwa lazima wao kuungana na jamii
nyengine za watanzania kudumisha amani na utulivu katika kipindi hiki cha
kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani ili kufanikisha jambo hilo
muhumi kwa mustakabali wa Taifa hili.
“Hakuna jamii isiyotambua umuhimu wa uchaguzi kwenye nchi
yoyote ile hivyo sambamba na hilo nyie ni watoa huduma mnapaswa kuacha
kujiingiza na masuala ya siasa kwa sababu wananchi wote wanategemea huduma zenu
bila kujali itikadi zenu “Alisema Mwenyekiti huyo.
No comments:
Post a Comment